Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Uhaba wa ajira ni changamoto kwa mwajiri na mtafuta ajira

Uhaba wa ajira ni changamoto kwa mwajiri na mtafuta ajira

Thu, 31 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kutokana na uhaba wa ajira hivi sasa vijana wamejikuta wakigombania fursa chache ambazo nazo hujitokeza mara chache hali inayosababisha waajiri nao kutokuwa na muda wa kutosha kufanya tathimini ya mtu wanayemtaka.

Utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi wa mwaka 2014 nguvu kazi ya Taifa nchini Tanzania ilikuwa watu 25,750,116, sawa na asilimia 57 ya watu wote Tanzania Bara. Aidha, kati ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi, walioajiriwa walikuwa watu 20,030,139 na wasioajiriwa walikuwa 2,291,785.

Leo hii shule ikitangaza nafasi za kazi kwa walimu wa sekondari na msingi kama nafasi zipo tatu si jambo la ajabu kukuta walioomba nafasi hiyo wanafikia 2,000, hiyo yote ni kwakuwa Serikali imepunguza kasi ya kuajiri huku wasomi nao wakiongezeka mtaani.

Kutokana na changamoto za ajira zilizopo sasa watu wengi wameibuka na ubunifu mbalimbali wenye lengo la kuwatengeneza watafuta ajira kuendana na soko lililopo lakini pia kuwakutanisha watafuta ajira na waajiri.

Mtendaji Mkuu wa kampuni ya BrighterMonday Tanzania ambayo hujifanya shughuli za kirasilimali watu Mili Rughani, anasema kutafuta wafanyakazi wenye sifa na uwezo unaohitajika ni zoezi ghali sana kwa waajiri wengi kwakuwa linapitia mlolongo mrefu hivyo mara nyingine mwajiri kujikuta anapata mfanyakazi asiye na vigezo stahiki.

Makampuni mengi yanayochipukia hupata wakati mgumu wakati wa kuajiri watu wanaoweza kuvusha kampuni hayo ili yawe makubwa. “Kumekuwa na ongezeko kubwa la uhitaji wa ajira miongoni mwa watu, Hivyo waajiri wanapotangaza nafasi ya kazi hupokea mamia ya maombi hivyo kuwa na changamoto kubwa ya kuchagua ni mwombaji yupi anaweza kufaa kwa ajili ya nafasi husika na shida hiyo ipo zaidi kwa makampuni yanayochipukia,” amesema Rughani.

Anasema kutokana na jambo hilo watu wenye majukwaa kama ya kwake wanahitaji kuwa wabunifu zaidi ili kuwasaidia wote watafuta ajira na watafuta rasilimali watu.

“Mfano sisi tunatumia mfumo wa kielektroniki uitwao Best Match ambao huratibiwa na maafisa rasilimali watu (HRs). Husaidia kupanga watafuta ajira kulingana na sifa na ubora wao na hivyo kumrahisishia mwajiri kuchagua mwombaji anayefaa kwa ajili ya nafasi husika,” anasema Rughani.

 

Columnist: mwananchi.co.tz