Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

UCHOKOZO WA EDO: Mheshimiwa Lukuvi sogea kidogo tupige soga

46392 Edo+kumwembe UCHOKOZO WA EDO: Mheshimiwa Lukuvi sogea kidogo tupige soga

Wed, 13 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kulala na njaa ni tatizo na usingizi hugoma ikitokea umelala bila kula. Juzi nililala na njaa. Nikakurupuka kutoka usingizini. Usiku wa manane. Nikasogea sebuleni kuwaza mambo mengi ya nchi yetu. Nikawaza mambo ya kijinga na ya msingi. Nikawaza jinsi ambavyo jiji la Dar es Salaam linavyoendelea kujaa.

Soma zaidi: UCHOKOZI WA EDO: Mioyo yetu ilishafunga mjadala wa Mo kitambo

Nikawaza jinsi Mbezi ya Kimara sasa ilivyoungana na Kibaha, Tegeta ilivyoungana na Bagamoyo, Mbagala ilivyoungana na Mkuranga, pia nikawaza jinsi Kigamboni inavyoweza kuungana na Zanzibar!

Kuna majumba ya kifahari ambayo yanajengwa nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Zamani maeneo ya nje ya jiji yalikuwa mashamba na misitu. Siku hizi ni makazi ya watu na waliohamia huko hawawezi hata kupumua. Hewa imeanza kukosekana.

Soma zaidi: UCHOKOZI WA EDO: Lowassa ametuziba wote midomo, tunaona aibu

Watu wanajenga sana. Matajiri na maskini wote wanajenga huko, huku wakati mwingine heshima ikikosekana. Unaweza kukuta muuza chipsi au kondakta wa daladala anajenga kando ya Mzee Andrew Chenge. Nchi yetu ina vurugu sana. Kila mtu anatafuta kiwanja na kujenga.

Soma zaidi:UCHOKOZI WA EDO : Mgeja amenikumbusha mbali, ‘ulipo tupo’

Unajiuliza, watu wa wizara ya waziri William Lukuvi wanajua kwamba tunahitaji uwepo wa huduma nyingine za kijamii? Kila siku tunagawiwa viwanja maeneo ya nje ya mji. Wizara ya baba Lukuvi wanajua kwamba inabidi yatengwe maeneo ya makaburi, makanisa, misikiti, maeneo ya wazi, viwanja vya michezo na huduma nyingine za jamii?.

Soma zaidi: UCHOKOZI WA EDO:Nabisha kwamba Prof Kabudi kateuliwa ‘kumdhibiti’ Lissu

Tumetafakari kwamba jiji letu litakua kwa kiasi gani kufikia miaka ya uzee wa wale akina ‘kamwene’ walioshinda tuzo za Azam majuzi? Kila siku watu wanavunjiwa nyumba zao kupisha ujenzi wa barabara, je tumejiandaa, tuna uhakika kwamba baadaye maeneo yote ambayo kwa sasa tunawapa watu viwanja hatutayahitaji kwa ajili ya ujenzi wa barabara na mambo ya msingi kwa matumizi ya Serikali?

Tumewahi kufanya makosa huko nyuma na sasa kuna vilio vingi vya uvunjwaji wa nyumba za wananchi, je tuna uhakika mambo haya hayatarudi tena? Napata hofu kila siku ninaposikia matangazo ya kuuzwa kwa viwanja bila ya kujua kwamba katika maeneo husika tunahitaji misikiti, makanisa, viwanja vya michezo na mambo mengine ya msingi kwa shughuli za umma.

Soma zaidi: UCHOKOZI WA EDO: Edward Lowassa ‘hajawahi’ kuwa CCM wala Chadema

Sogea karibu mheshimiwa Lukuvi tutete kuhusu jambo hili. Binafsi nakukubali. Nakumbuka ulikuwa mgeni wa heshima katika sherehe za mahafari yangu pale Shule ya Sekondari Jitegemee miaka ile ya zamani.



Columnist: mwananchi.co.tz