Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

UCHOKOZI WA EDO: Tungewasikiliza na wateja wa juisi ya tende Zenji

70600 Edo+kumwembe

Fri, 9 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tangu lini nchi yetu ikaishiwa vituko? Siku mbili zilizopita kuna rafiki yetu kule Zanzibar ametiwa ndani. Kosa? Anatuhumiwa kuuza juisi ya tende ambayo inadaiwa ndani yake inatiwa viagra. Wanaume wanaikimbilia. Wanaisifu vilivyo. Hatimaye ameshtukiwa.

Hatujui kosa lake litakuwa lipi. Labda la udanganyifu. Ndiyo, labda la udanganyifu wa kuaminika. Hili jambo ni gumu kwa sababu nahisi hata wateja watatamani wamuwekee dhamana ili waendelee na utaratibu wake wa ‘kuokoa nyumba’ zao.

Nadhani Maafande wangepitisha kura kwanza kuuliza kama wateja wamekasirika na kushtushwa na tukio zima. Si ajabu wangekutana na wateja wenye furaha ambao wangeshangazwa kuona muuzaji wa juisi ametiwa ndani.

Tukio hili limenikumbusha simulizi ambayo niliwahi kuambiwa kule Afrika Kusini. Vijana wa Kitanzania waliwahi kwenda kule na ujanja huu huu ingawa kwa njia tofauti. Afrika Kusini ni moja kati ya nchi ambazo watu wake wengi wameathirika na tatizo la nguvu za kiume.

Kuna vijana wajanja wakaamua kwenda na staili ya kusaga tembe za viagra na kuziingiza ndani ya vipande vikavu vya miti ambayo waliita dawa.

Wazulu walikuwa wanatafuna vipande hivyo na kujikuta wakirudi katika nguvu zao za kawaida, tena maradufu.

Pia Soma

Vijana wa Kitanzania walikuwa wakiendesha magari ya kifahari mitaa ya Durban, Johannesburg, Pretoria na kwingineko kwa sababu hii. Walipata pesa nyingi. Ni kama ambavyo nadhani rafiki yangu pale Zanzibar alijikuta akitengeneza pesa nyingi kuliko wenzake katika biashara hii ya juisi.

Tatizo ni kwamba yeye alijikita zaidi katika ‘kuwa-suprise’ wateja ambao hawakuhitaji dawa hiyo moja kwa moja.

Wenzake kule Sauz walikuwa wanafanya moja kwa moja biashara ya dawa ingawa ilikuwa katika ujanja wa hali ya juu.

Matatizo ya nguvu za kiume yanapoelekea tunaweza kuambiwa nyama ya mjusi ni tiba na bado tukaigombea. Nasubiri kusikia upande wa wateja wa Zanzibar unasemaje kuhusu juisi ya tende.

Columnist: mwananchi.co.tz