Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

UCHOKOZI WA EDO: Tunaenda kuteketeza noti nyingine Singida

65003 Edo+Kumwembe

Tue, 2 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Usijali sana unaposikia kwamba mkuu wa jengo la Dodoma hajui mbunge wake aliyepigwa risasi yuko wapi. Usijali sana. Kitu cha kujali ni pale anapofungua mdomo na kusema ‘Nimeamuru mwenyekiti wa tume ya uchaguzi aitishe uchaguzi katika jimbo lake’.

Hii ni kauli ya mwanasiasa, kama ingekuwa kauli ya mchumi yeyote yule angeweza kuweka wazi zaidi kwamba ‘Tumeamuru tutumie zaidi ya shilingi bilioni moja kwa ajili ya jimbo ambalo litatugharimu tena shilingi bilioni moja miezi 10 ijayo kwa sababu ile ile’.

Hapa ndipo ambapo Taifa limekwama. Mambo mengi yapo kisiasa. Sheria nyingi zipo kisiasa. Tungezitafsiri kiuchumi tungeokoa mambo mengi. Hata hivyo nchi za dunia ya tatu hazijali sana mambo ya uchumi. Zinajali siasa huku zikibembeleza wananchi wake na maneno matamu ya kulainisha ya ‘kujali sana wanyonge’.

Ukiuliza sana kwanini tusitengeneze sheria ambazo hazitaruhusu chaguzi za marudio kijingajinga utaambiwa ‘Demokrasia ina gharama zake’. Wakati una hofu Namba Moja atapata wapi pesa za kugharamia miradi mingi mikubwa aliyoanzisha, upande mwingine hauna hofu na matumizi ya namna hii ya chaguzi za marudio.

Kikubwa kinachobaki kwa sasa ni kupiga hatua mbili mbele, kisha hatua tatu nyuma na kupiga makofi ya kujipongeza. Katika hali halisi hakuna kitakachobadilika katika majimbo ya waliounga mkono juhudi au wanaoumwa, au walioamua kuwa watoro wa makusudi bungeni. Tunapiga siasa tu. Hata kama majimbo yao yangekuwa tupu mpaka mwisho wa awamu ya kwanza bado umaskini wetu utabakia pale pale. Kinachofanyika ni kuendelea kujitia umaskini usio na sababu kwa maamuzi yenye msingi wa kisiasa.

Waliotengeneza hizi sheria wanashangilia kwa sasa. Hawataki ziondoke kwa sababu kama hizi. Mwisho wa siku zinatudhihirishia tu jinsi tulivyo, jinsi ambavyo tupo bize na maneno matamu ambayo hayataondoa umaskini wetu.

Pia Soma

Unapoona tunakwenda katika uchaguzi wa marudio huku tukitegemea kufanya mwingine ndani ya miezi 10 tu ijayo, halafu kuna watu wanagonga meza kwa nguvu pale Dodoma, unapata shaka na uwezo wa kufikiria wa watu wanaotoa maamuzi mazito katika nchi hii.

Columnist: mwananchi.co.tz