Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

UCHOKOZI WA EDO: Spika anapowasahau kwa makusudi wale wasemao ‘ndiyooo’

Thu, 20 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Jana tu nilikutana na spika wangu akiwa katika foleni pale Ubungo. Mbele yake kulikuwa na gari linalopiga king’ora. Nikajua anawahi hafla ya uwekaji jiwe la msingi kwa ajili ya upanuzi na ujenzi wa barabara ya njia nyingi ambazo zinatarajiwa kuanza kujengwa hivi karibuni kuanzia Kimara hadi Kibaha.

Nikatabasamu kumuona spika wangu katika suti maridadi. King’ora mbele yake. Maisha yanataka nini zaidi? Nikatabasamu tena. Nikamsubiri kwa hamu kumsikia akiongea kama miongoni mwa watoa hotuba pale Kimara, jana.

Kuna mambo niliyategemea. Kisaikolojia, mwanadamu anayepishwa barabarani, trafiki anavuta magari katika foleni yake ili yeye apite, nadhani vitu vingi vya kipinzani hawezi kuvipenda. Amezoea kupita katika barabara isiyopingwa, vipi aone mambo yanayopingwa?

Nilimsikia spika akieleza wazi kwamba pale mjengoni kwake watu wanaoitwa wapinzani wanapinga kila kitu. Inawezekana kabisa anasema kweli, lakini kuna wale wa upande mwingine ambao kila kitu wanasema ‘ndiyooo’. Hawa hakuwataja.

Hili ndilo tatizo langu la msingi. Kuna wanaosema ‘ndiyooo’ kwa kila kitu na wasemao ‘hapanaaa’ kwa kila kitu. Kwa nini spika alichagua kuwasema wanaosema hapana tu?

Hawa wanaosema ndiyo kwa kila kitu wamemchanganya hata namba moja wetu. Wakati mikataba ya ovyo ya madini ilipopelekwa mjengoni walisema ‘ndiyooo’ kwa kila kipengele. Wakati namba moja kaingia madarakani akapinga mikataba hiyo hiyo wakasema ‘ndiyooo’. Spika hawa hawaoni kama tatizo?

Kwa mfano, wanaosema hapana mpaka leo hawana nguvu ya kuamua pamoja na hiyo hapana yao. Wanaosema ‘ndiyooo’ wana nguvu ya kuamua. Leo namba moja wa nchi hii anatuambia kwamba nchi iliharibiwa sana, ni kweli, je iliharibiwa na wale waliokuwa wakisema ndiyo kwa kila kitu au hapana kwa kila kitu?

Ukijaribu kuusoma moyo wa namba moja nadhani kimyakimya anawachukia sana waliokuwa wakisema ‘ndiyooo’ kwa kila kitu hata katika mikataba ile ya madini.

Namba moja akifungua makabrasha mbalimbali ya nchi hii ni wazi kwamba anasononeshwa sana na wale wasema ‘ndiyooo’ hasa wa tawala zilizopita. Hawa wasema ‘hapana’ wanamsumbua kwa sasa lakini sio kiini cha matatizo aliyoyakuta katika utawala wake.



Columnist: mwananchi.co.tz