Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

UCHOKOZI WA EDO: Siku mbili tofauti Coco Beach na Barcelona

57102 Edo+kumwembe

Mon, 13 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tuongee mambo magumu au mepesi? Tuongee habari zilizotokea msibani pale Kilimanjaro au tuachane nazo? Nadhani tuachane nazo.

Tufanye mambo yawe mepesi kama hapa Hispania nilipo katika mji wa Barcelona.

Ukisia Barcelona kwa haraka haraka unaweza kudhani nataka kuongelea habari za kina Lionel Messi. Hapana.

Kuna maisha mengine nje ya habari za soka ndani ya Barcelona. Tena ni maisha yenye mvuto zaidi.

Ndani ya ndege kutoka Geneva kwenda Barcelona unashangaa Wazungu wanavyosisimkwa kwenda Barcelona.

Tunashuka uwanja wa Ndege wa Barcelona Wazungu wanampigia makofi rubani. Wameshafika Barcelona.

Pia Soma

Ukiwadodosa wanakueleza kuwa wanafurahia hali ya hewa. Kwao ni baridi sana. Barcelona kuna joto. Lakini zaidi ya kila kitu wanasifia fukwe za Barcelona. Ndizo ambazo zimewaleta.

Hapo unakumbuka mambo mawili. Kwanza kabisa, kati ya kitu kibaya katika maisha ni kuzungukwa na majirani masikini.

Raia wa Zambia, Uganda, Kenya, Rwanda, DR Congo wangeweza kutiririka nchini kwenda katika fukwe zetu kama nao wangekuwa ni raia wa nchi za kitajiri. Usiombee kupakana na masikini wenzetu ambao akili zao zipo katika vita na ubabe.

Uwanja wa Ndege wa Barcelona hakuna maswali. Hakuna urasimu. Wanajua wageni wameleta fedha. Mitaani baa zinafungwa saa kumi usiku. Raia wa kigeni wanazurura kwa amani wakiimba na kunywa. Hakuna ‘defenda’ za Polisi zinazowasumbua. Zinawajua wameleta fedha.

Polisi wanafanya kazi yao kwa kutumia ‘intelejensia’ ya ukweli na uhakika. Ukikutana na polisi unahisi amani zaidi. Sitaki kuzungumza kuhusu kwetu.

Mwishowe serikali ya Barcelona inapiga fedha tu kwa kutumia neno utalii. Hasa ule utalii wa uwepo wa joto katika nchi yao pamoja na fukwe. Ni vitu ambavyo Tanzania vipo.

Tatizo kuzungukwa na masikini wenzetu. Tatizo hizo fukwe zenyewe zilivyo chafu. Hata sisi wenyewe hatuna muda wa kwenda. Lakini jiulize jinsi ambavyo ukikutwa ufukweni usiku unavyoulizwa lile swali na polisi. ‘Unafanya nini ufukweni usiku huu?’ Unashangaa. Inamhusu nini zaidi ya kunilinda? Lakini unaishia kumsamehe tu kimoyomoyo kwa sababu hata Serikali haijakulinda. Kwa nini haijakuwekea taa nyingi ufukweni kama Barcelona? Tunahitaji kujifunza.

Columnist: mwananchi.co.tz