Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

UCHOKOZI WA EDO: ‘Sauzi’ kutamuachia maswali mengi Namba Moja

59955 Edo+kumwembe

Tue, 28 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Ijumaa, Namba Moja alipanda ndege yake kwenda Afrika Kusini ‘Sauzi’. Pengine ni safari ya mbali zaidi tangu aingie madarakani. Pia, ni safari ya mbali zaidi akitumia usafiri alioununua mwenyewe. Kuna watu wameshaipanda ndege yake zaidi ya mara 10 tofauti na yeye. Akina Masanja Mkandamizaji kila siku tunawaona Instagram wakiwa katika ndege yake.

Mwanadamu ameumbwa kusahau. Kama Namba Moja aliwahi kufika Sauzi hapo zamani, nadhani inawezekana alikuwa amesahau uzuri wake ulivyo. Atakuwa ameukumbuka tena baada ya kutua katika Uwanja wa ndege wa Oliver Tambo.

Huwa naenda Sauzi mara nyingi. Naamini Sauzi itamuachia maswali mengi Namba Moja. Kwanza itazidisha hasira zake dhidi ya umaskini. Hasira dhidi ya barabara zetu mbovu. Atakuwa amepita katika ‘fly over’ zaidi ya 500 katika mizunguko yake ya hapa na pale Johannesburg na Pretoria.

Atakuwa amepita katika zile barabara ambazo tano zinakwenda, tano zinarudi. Atapata hasira kali. Namjua Namba Moja. Yote haya ataona yanawezekana nyumbani. Wasauzi wametumia vizuri madini kuijenga nchi yao. Kwa nini sisi tushindwe?

Kitu kimoja kitamchanganya Namba Moja. Yote yale yaliyofanyika pale Sauzi yametokana na akili za mtu mweupe. Kaburu. Hawa ni watu ambao wakati fulani wanaitibua akili ya Namba Moja. Anaamini tunaweza kwenda bila ya wao.

Watu weusi wa Sauzi wangeweza kuifanya nchi hiyo iwe kama ilivyo? Nimeishi nao, sidhani. Wasingeweza. Namba Moja yuko sahihi kuzuia dhuluma ambazo wanatufanyia kule migodini na kwingineko. Hata hivyo, akipepesa macho zaidi atagundua kwamba bado kuna umuhimu wa kukaa nao vizuri na kuiendeleza Tanzania. Sisi tulioishia darasa la saba tunasikia wasomi wakidai kwamba hii ni ‘win win situation’. Wao wale na sisi tule.

Pia Soma

Wao kutokula kabisa kutoka kwetu ni ngumu. Na sisi kwenda wenyewe bila ya wao ni ngumu. Bila kudanganyana, Sauzi ni kipimo sahihi cha utofauti wa fikra kati yao na sisi. Namba Moja atajikumbusha hivyo. Amekwenda kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa Sauzi, Cyril Ramaphosa lakini ukweli ni kwamba akina Ramaphosa wameachiwa nguvu za kisiasa tu. Nguvu za kiuchumi zinaendeshwa na watu weupe.

Columnist: mwananchi.co.tz