Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

UCHOKOZI WA EDO: Nazidi kutafakari ugomvi wetu na wazungu

32115 Uchokozipic TanzaniaWeb

Tue, 18 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Nimeshuka katika ndege juzi nikitoka Afrika Kusini. Huwa naenda kule mara nyingi. Juzi ikawa mara yangu ya kwanza kurudi mnyonge. Nimerudi na mawazo. Watu wanaoitwa wazungu wanazidi kunichanganya kila kukicha.

Mara nyingi nikiwa Afrika Kusini huwa nawatazama tofauti wazawa wa nchi ile. Wengi wao wanaonekana ni wavivu, walevi. Husubiri Ijumaa ifike wakalewe. Husubiri mwisho wa mwezi ufike wakafanye balaa mitaani wakiwa na visenti vyao. Akili ya kufikiri na kutenda wamemwachia mzungu. Kaburu!

Mwisho wa mwaka ‘waswahili’ kule wanaishi kama wachaga. Wengi huondoka mijini na kurudi makwao. Sasa hivi jiji la Johannesburg liko tupu. Hakuna foleni barabarani. Maeneo ambayo angalau yana watu wengi ni baa na katika maduka makubwa (Malls).

Rafiki zangu fulani ndio wamenifanya nijihisi mnyonge. Wameniambia kwamba ifikapo Desemba, wafanyakazi wa Serikali hulipwa mshahara mara mbili. Nikachanganyikiwa na kujiuliza ni Afrika hii hii! Baadaye nikagundua ni Afrika yenye mchanganyiko na Ulaya ndani yake.

Baadaye nikajipa majibu mawili. Afrika Kusini ni nchi ya wazungu. Walifika mwaka 1652. Nikajiuliza, bila ya wao leo wafanyakazi wangeweza kulipwa mishahara miwili ifikapo Desemba? Sidhani. Sidharau rangi yangu wala bara langu, lakini nionyesheni nchi nyingine nje ya Libya ya Muammar Gaddafi na nchi fulani za Kiarabu ambazo zingeweza kufanya hivyo?

Watu weusi tuna matatizo fulani hivi ya kihistoria na kiasili. Au labda tulifanywa kuwa hivi? Nikawaza kitu kingine, hapa tulipofika tunaweza kweli kwenda mbele bila ya kushirikiana nao au kwenda nao sambamba?

Namba moja wetu amekuwa akiwaza hivi lakini nadhani inabidi awaze mara mbili. Kuna mambo mawili hapa. Kwanza kuna mwanzo mbovu wa kihistoria, pili wamejaribu kuitengeneza dunia kuwa yao. Afrika Kusini ni mfano halisi wa tofauti ya mzungu na mtu mweusi.

Mara nyingi nawaza kama wale weusi wa Afrika Kusini wangeweza kulipana mishahara mara mbili kama mzungu asingekwenda huko. Nawaza jinsi ambavyo baada ya kina Jacob Zuma kukabidhiwa nchi kulivyoibuka madai ya kufanyika ufisadi wa ajabu. Wangeweza kweli kugawana mishahara mara mbili mwisho wa mwaka?

Nchi za Asia zinakwenda kasi. Sisi kasi yetu na nidhamu ya rangi yetu kama ile ya kaka Kabila na viongozi wenzake wengi wa Afrika, tunaweza kwenda sambamba na mzungu? Nimewaza sana. Nikayakumbuka hadi mabango ya baba zangu inapowadia sikukuu ya Mei Mosi.



Columnist: mwananchi.co.tz