Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

UCHOKOZI WA EDO: Msikilize mzungu anayeamini ataliwa na wanadamu Afrika

56418 Edo+Kumwembe

Thu, 9 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

TUNAPOZA kichwa leo. Mambo mengi magumu yamepita hapa karibuni ikiwemo msiba wa Mzee Mengi. Tunapoza kichwa kidogo leo. Bado nazurura Ulaya. Majuzi nilikuwa katika mji mdogo wa Genk, kwa sasa ni nyumbani kwa staa wa Tanzania, Mbwana Samatta anayecheza katika klabu ya Genk.

Tukaanza kupiga soga. Jinsi anavyoyaona maisha ya Ulaya. Uzoefu wake kwa miaka mitatu ya kuishi Ulaya. Baadaye nikamuuliza swali la kawaida ambalo jibu lake lilinifanya nitafakari namna ya kuitangaza upya Tanzania kule Ulaya.

Nilimuuliza, Wazungu wana mtazamo gani kuhusu Tanzania na Afrika kwa ujumla? Jibu lake nilicheka sana. “Kuna Wazungu walioelimika na kusafiri. Lakini, kuna Wazungu ambao hawajaelimika na kusafiri. Hawa ndio ambao wanadhani Afrika tunaishi na wanyama mitaani. Unajua kwa nini? Sisi huku huwa tunawaambia kwamba wakija Afrika wataona wanyama wengi tu. Sasa huwa wanadhani tunaishi na wanyama mitaani” alisema Samatta.

“Kuna mchezaji mwenzetu mmoja ambao sisi wachezaji wa Afrika tunaocheza Gnk tuliwahi kumtisha. Tulimwambia kwamba akija Afrika tutamla. Tutamfanya mboga. Aliogopa sana akaapia kwamba hatakuja Afrika. tulicheka sana. Nadhani aliamini hivyo”.

Kufikia hapo nikaanza kutafakari. Inawezekana kuna Wazungu hawaji Afrika kwa sababu wanaamini Waafrika ni kama wanyama. Kwamba kuna maisha duni yaliyopitiliza na hakuna hoteli kubwa kama zile za ufukweni kwetu bara na Zanzibar?

Kumbe inawezekana tunakosea sana kutangaza wanyama peke yake bila ya makazi ya wanadamu wa eneo husika. Hawaamini kwamba tuna hoteli ambazo wao hawana. Hawaamini kwamba tunakula ‘breakfast’ nzito kama wao.

Habari zinazohusiana na hii

Inanikumbusha mwanamuziki maarufu wa Marekani, 50 Cent alipokuja nchini. Tulienda kufanya naye mahojiano pale Kilimanjaro Hoteli na muda wote alikuwa anashangaa uzuri wa hoteli. Alidai kwamba hakujua kama Tanzania kunaweza kuwa na hoteli nzuri kama ile. Ni wazi kwamba kama aliishia pale na kurudi uwanja wa ndege kwa ajili ya kurudi kwao hakujua kama kuna hoteli nyingine nzuri zaidi ya ile.

Tunaweza vipi kumpata huyu mchezaji ambaye anaamini akija Afrika ataliwa na wanadamu wenzake? Bodi ya Utalii kazi wanayo. Wabadilishe mtazamo. Wasitangaze Wanyama peke yao. Kuna kazi ya kutangaza maisha yetu pia.



Columnist: mwananchi.co.tz