Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

UCHOKOZI WA EDO: Mkoa wa Mara nitaendelea kuusikia redioni

70099 Edo+kumwembe

Tue, 6 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mara ipo Tanzania kweli? Ukiuliza hivi utajibiwa ‘ndiyo’. Na hata Jiografia ipo hivyo. Hata baba wa Taifa letu alizaliwa Mara. Hakuna ubishi wala ubaguzi. Ipo Tanzania. Kwa nini watu wake wapo kama walivyo? Inashangaza kidogo.

Pande zote za Tanzania ubindamu umepungua, lakini ukisikiliza mikasa ya mkoa wa Mara unabakia mdomo wazi zaidi. Utu umeondoka kwa kasi zaidi. Huwa namsikiliza Mkuu wa Mkoa ule pamoja na Kamanda wake wa mkoa wakitapatapa kuelezea mauaji ya kikatili mara kwa mara.

Juzi, nikasikia kisa cha kijana aliyenyimwa bia katika sherehe. Akapotea kwa muda katika eneo la tukio akiwa na dhamira yake moyoni. Akarudi na mishale na kuanza kuwateketeza ‘wabaya’ wake. Kisa? Kunyimwa bia. Na kumbuka kabla ya hapo alishakunywa mbili kabla ya wageni waalikwa hawajafika. Ubaya ulikuja alipoambiwa asinywe tena mpaka wageni wafike. Hiki ni kisa tosha cha kuja kurushia watu mishale?

Nikasikia kisa cha kijana mwingine aliyemkata rafiki yake mapanga na kumuua kutokana na deni la Sh2,000. Mara kweli ipo Tanzania? Halafu kuna huyu ambaye siku tatu zilizopita aliamka asubuhi akiwa na mapanga mawili mkononi na kuua familia yake. Alichana viungo vyao kabisa. Sijui alikuwa na hasira ya nini.

Kila unapofungua redio au televisheni kusikiliza taarifa ya habari unakutana na mambo mawili. Kama sio kukamatwa kwa bangi, basi utasikia mauaji yaliyohusisha silaha kali ama panga au mshale. Mara imekwama wapi?

Wiki mbili zilizopita nikasikia kijana aliyemuua mpenzi wake kwa mapanga. Kisa? Kaunguza mboga. Mara hakuna adhabu nyingine ya kawaida zaidi ya kukatwa mapanga? Sijui. Mikoa mingine yanafanyika mambo ya kikatili pia. Hata hivyo, vyanzo vya mauaji hayo ni tofauti kabisa na vyanzo vya mauaji ya mkoa wa Mara.

Pia Soma

Kuna mikoa sijawahi kugusa hii nchi. Mara, Singida, Tabora, Kigoma. Rukwa na michache mingineyo. Natamani siku moja nifike nifanye utalii wa ndani. Hata hivyo, kati ya mikoa yote hii, naomba mkoa wa Mara niendelee kuusikia redioni tu na kuutazama katika televisheni. Naomba wageni mnaokwenda huko mniwakilishe.

Columnist: mwananchi.co.tz