Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

UCHOKOZI WA EDO: Chenga maridadi ya Maalim imetuachia maswali

47763 Uchokozipic

Thu, 21 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tulioishia darasa la saba juzi tukapeleka sikio letu mahakamani. Ghafla Maalim Sief chalii. Tukawatazama sura za pande zote mbili. Walioshinda walitabasamu. Walioshindwa wakatabasamu. Kwa nini? Tukawaza.

Kumbe kulikuwa na mpango maalumu. Ghafla Maalim Seif na watu wake wakahama chama chao. Wakaenda kwa Zitto Kabwe. Pamoja na akili zetu za darasa la saba tukajua tu kwamba haikuwa bahati mbaya. Walipanga siku nyingi tu. Sawa, hatukwenda shule lakini hamuwezi kutudanganya kirahisi.

Kilichofuata ndio kimetuacha midomo wazi zaidi. Kwa nini wale wa kijani wamenuna Maalim kwenda kwa Zitto? Jibu ni moja tu, nyumba ya adui ikiungua unapenda iungue tu siku zote. Kuondoka kwa Maalim kunamaanisha kwamba kwa sasa hakuna nyumba inayoungua.

Ina maana tunakwenda katika kipute cha 2020 bila ya nyumba yoyote kuungua. Nadhani wangependa Maalim ang’ang’anie ili aendeleze kupoteza muda na kuunguza nyumba. Maalim alishashtukia kwamba atapoteza muda.

Kingine ambacho kimefuata na kimetuacha midomo wazi sisi tulioishia darasa la saba ni namna ambavyo wale jamaa wengine wanaopoteza majimbo kila kukicha walivyoona hakuna tatizo kwa Maalim kutokwenda kwao na kuamua kwenda kwa Zitto.

Yule jamaa anauguza viungo vyake vya mwili katika nchi anayocheza Mbwana Samatta na hajaona tatizo kabisa. Siasa bwana!. Nlidhani wale jamaa wangekasirika kwa nini Maalim hajaenda kwao? Hawakukasirika. Walichotaka ni kwamba Maalim aondoke tu kule alikokuwa.

Siku hizi hawana tatizo na Zitto. Kama hawana tatizo na Zitto kwa nini wawe na tatizo na Maalim?. Naamini wanajua kwamba mbele ya safari wataungana tu kwa ajili ya kipute cha 2020. Nafikiri ndio lile Azimio la Zanzibar.

Nadhani vyovyote vile ilivyo Maalim atabakia kuwa na nguvu katika maeneo yake yale yale. Awe katika jezi yoyote ile wafuasi wa Maalim wanabakia kuwa wale wale, na kwa sababu wameona mbele ya safari watakuwa na Maalim basi sio lazima aje kwao au aende kwa Zitto.

Tunasubiri tu kuona wale wengine wamejipanga vipi dhidi ya Maalim. Labda imekuwa ghafla sana kwa Maalim kuvua jezi. Walitazamia aendelee kugombania ngalawa lakini amejitosa kwingine. Wale watoto wa Shilawadu huwa wanasema ‘Mambo ni mengi muda ni mchache’. Wapo sahihi.



Columnist: mwananchi.co.tz