Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

UCHAMBUZI: Ya DC Kasesera na miaka 42 ya CCM

40344 Elius+Msuya UCHAMBUZI: Ya DC Kasesera na miaka 42 ya CCM

Wed, 6 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kauli ya Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesera kuhusu madiwani waliohamia kutoka upinzani haiwezi kupita bila kujadiliwa.

Alikuwa akiwajibu makada wa CCM wilayani humo waliohoji sababu ya madiwani waliohamia CCM wakitoka vyama vya upinzani kupitishwa moja kwa moja kugombea bila kufuata utaratibu wa chama wa kuwashindanisha ili kupata mgombea aliyekubalika.

Kasesera alisema waliamua kuwaachia madiwani wa upinzani wagombee bila kupingwa ikiwa ni moja ya makubaliano ya wao kuhamia na walikubali kwa sababu ulikuwa ni mpango wa chama kuhakikisha kata zote zinarudi CCM.

Kwa kuwa kauli hiyo haijapingwa na uongozi wa chama hicho, inaonekana Kasesera ameeleza ukweli wake, japo wakati mwingine wasingependa ujulikane.

Hadi mwisho wa mwaka jana kulikuwa na zaidi ya madiwani 140 kutoka vyama vya upinzani waliohamia CCM, wengi wakisema wanaunga mkono juhudi za Rais kuleta maendeleo.

Kulikuwa pia na wabunge 10 kutoka vyama hivyo waliorejea kwa sababu hiyohiyo na wote wamerudi kwenye majimbo yao.

Katiba ya CCM toleo la mwaka 2017 kifungu cha 52(7b) kinaipa mamlaka kamati ya siasa ngazi ya kata kufikiria na kutoa mapendekezo yake kwa kamati kuu ya siasa ya halmashauri ya wilaya juu ya wanachama wanaoomba udiwani.

Kifungu hicho kimerekebishwa kutoka kwenye matoleo yaliyopita ambayo yalitoa demokrasia kwa wajumbe wa ngazi ya kata kupiga kura kwa wanaoomba kugombea. Diwani ni mwakilishi wa wananchi katika kata husika bila kujali ametoka chama gani. Ikiwa diwani huyo hakubaliki kwenye chama anachotoka au pengine kule alikoasi ameacha mazingira mabaya, anakwenda kumwamkilisha nani?

Kwa mtindo huu, kuna wananchi wengi wanaoongozwa na watu wasiowaridhia, bali ni kutokana tu na matakwa ya chama chenye tamaa ya kurudisha kata zote zilizokuwa upinzani, ndio kisa baadhi walikataliwa katika kura za maoni.

Suala la kukataliwa kwa madiwani wanaotoka upinzani lilianzia Arusha mapema mwaka 2017 ambapo madiwani watatu kutoka Chadema walianguka kwenye kura za maoni. Hata hivyo, uongozi wa juu wa CCM Mkoa uliwapa nafasi licha ya kushindwa uchaguzi.

Je, hiki ndiyo kipaumbele cha CCM ambayo kwa sasa inatimiza miaka 42 tangu kuasisiwa kwake? Kipaumbele ni kujaza wabunge na madiwani hata kwa njia ya mkato au ni kuwaletea maendeleo wananchi?

Ukiangalia historia ya mfumo vingi vya siasa tangu ulivyorejeshwa mwaka 1992, CCM imekuwa ikishinda nafasi ya urais, idadi kubwa ya wabunge na madiwani.

Hata katika uchaguzi wa mwaka 2015, CCM ilipata wabunge na madiwani wengi kuliko upinzani. Je, bado CCM inahitaji wabunge na madiwani wangapi ili ijiweke katika nafasi ya kuleta maendeleo ya wananchi?

Haidhuru, kwa kuwa uchaguzi ni ushindani basi kanuni za ushindani lazima zifuatwe, tangu ndani ya chama.

0754 897 287



Columnist: mwananchi.co.tz