Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

UCHAMBUZI: Siyo ushoga wala unga, tatizo liko hapa kwetu

33480 Levy Mwananchi Photo

Thu, 27 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Ni wazi kwamba lazima kuwepo na mikakati na juhudi zao makusudi ili kupiga kasi ya kutosha kuondokana na matatizo tuliyokuwa nayo. Na juhudi hizo ni kujipatia maarifa mengi yatakayotufaa katika nyanja mbalimbali za maisha yetu.

Na njia sahihi ya kusambaza maarifa ni kupitia malezi ya watoto wetu. Dunia ya leo inaendeshwa kwa maarifa, na kwetu tatizo sio maarifa bali tatizo ni namna ya kufikisha maarifa hayo kwa jamii inayotuzunguka. Ni kama tumekuwa nzige kwenye mazao.

Kama jamii tuna utaratibu gani wa kusambaza maarifa hayo? Je, elimu ya darasani inatosha kupima namna mzazi au mlezi anavyompa mwanae maarifa? Hata wanamuziki wanaodaiwa kupotosha jamii kwa nyimbo zao, wao pia walipotoshwa na wazazi wao.

Tangu mtoto anapoanza kutambaa, kutembea, na kuzungumza. Mwongozo kwa mzazi wa Kibongo bila kujali tajiri au masikini, umuongoze ili kumpa mtoto maarifa yanayoendana na umri wake. Hata ushoga unakua kwa kasi kutokana na kukosa miongozo bora.

Tuweke viwango kwamba mtoto kulingana na ukuaji wake ajue hiki baada ya kile. Ukweli ni kwamba hatuwezi kukuza uelewa wa mtoto wa Kibongo bila malezi bora na mpangilio sahihi wa kumjaza uelewa. Kifupi Bongo tunazaliwa kama binadamu na kulelewa kama wadudu.

Kila mzazi apewe mwongozo. Atakaoufuata, akiwa mbunifu zaidi ni vyema. Mwongozo uwe wazi na fasaha kwa wazazi na walezi katika hatua ya ukuaji wa mtoto. Ufafanue katika kila umri wa mtoto, mzazi ajitahidi mtoto wake ajue vitu kadhaa. Tupunguze mateja mitaani.

Kwa kudhani malezi ni kumfundisha mtoto matumizi ya ‘simu janja’. Ni kulizika taifa bila sanda. Kama taifa tunazalisha takataka tukiziita watu. Hata kutojua umuhimu wa kulipa kodi ni matokeo ya kukosekana mwongozo wa malezi. Malezi bora ndo kila kitu.

Faida ya sera ya taifa ya malezi ni kukuza uelewa wa mtoto wa Kitanzania. Bila hivyo tutaendelea kuzalisha kina Amber Rutty wa kutosha mitaani. Na kaletewa nyimbo zenye mashairi kerefu kila siku. Kwa sababu wote hawa kama makuzi yao walikosa malezi sahihi.



Columnist: mwananchi.co.tz