Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

UCHAMBUZ: Lissu anataka majibu, umma unataka majibu

40392 Pic+lissu UCHAMBUZ: Lissu anataka majibu, umma unataka majibu

Thu, 7 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Nimemsikiliza Spika Job Ndugai kuhusu hoja za Tundu Lissu na nikasoma andiko la Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani kuhusu kauli za Lissu, maelezo yote hayo hayajajibu kikamilifu hoja za mbunge huyo wa Singida Mashariki.

Kitendo cha taasisi zenye wajibu wa kujibu kutojibu kikamilifu hoja hizo, ndio maana ninasema si Lissu pekee anayehitaji majibu ya maswali yake, bali hata umma unataka kujua ukweli ni upi.

Lissu anachosema ni kuwa kifungu cha 24(1) cha sheria ya uendeshaji wa Bunge ya 2008 na marekebisho yake ya 2015, kinaeleza kuwa mbunge atatibiwa ndani au nje ya nchi kwa gharama za Bunge, lakini yeye tangu ashambuliwe kwa risasi Septemba 7,2017 mjini Dodoma, Bunge halijagharamia matibabu yake, si Nairobi, Kenya wala Brussels, Ubelgiji kama sheria inavyotaka.

Spika akasema tangu Septemba 7, 2017, Bunge limempa Lissu malipo mbalimbali yanayofikia Sh250 milioni ikiwa ni stahili zake mbalimbali Sh207.8 milioni, na Sh47 milioni za michango binafsi ya wabunge zilizotumika kwa matibabu nchini Kenya.

Katika ufafanuzi huo, Spika akasisitiza kuwa kuanzia sasa ofisi yake itaanza kumjibu Lissu, kwamba akiongea ni lazima wamjibu na kama atabisha hajapokea malipo hayo, atakuja na “mkeka” kujibu.

Lissu anasema malipo hayo ya Sh207.8 milioni ni mishahara na posho zake ambazo analipwa kwa mujibu wa sheria, ambayo ni haki ya kila mbunge na Sh43 milioni ni michango ya wabunge.

Sasa ufafanuzi wa Spika ndio unaongeza utata zaidi na umma unataka kufahamu, je, kweli Bunge kama taasisi, liliwahi kugharamia matibabu ya Lissu ndani na nje ya nchi kama sheria inavyosema?

Je, michango ya wabunge iliyofanywa kiubinadamu, inaweza kuchukuliwa kuwa ndio imetolewa na Bunge kama taasisi kugharamia matibabu ya Lissu, au Bunge nalo liliwahi kutuma fedha tofauti?

Ikumbukwe katika Bunge la Bajeti mwaka 2018, Spika alikaririwa akisema Bunge lisingeweza kugharamia matibabu ya Lissu kwa sababu alikwenda Nairobi na baadaye Ubelgiji bila kupata kibali.

Kama huo ndio ulikuwa msimamo wa Bunge, ni lini ulibadilika ili sasa Watanzania tuamini kwamba Sh250.8 milioni alizolipwa Lissu zilijumuisha gharama za matibabu zilizobebwa na Bunge kama mhimili.

Hoja nyingine ya Lissu ilikuwa ni kutokamatwa kwa mtu hata mmoja kuhusiana na tukio la kushambuliwa kwake, na kuwa walinzi hawakuwepo siku hiyo na kamera za CCTV ziliondolewa baadaye.

Lakini Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Dk Abdallah Posi anasema ili upelelezi makini ufanyike, vyombo vya uchunguzi vilihitaji kumpata Lissu na dereva wake ili waweze kuelezea nini kilitokea.

Ninajiuliza maswali na umma unajiuliza maswali, hivi mwathirika wa tukio la jinai akiwa mahututi kwa miezi mitatu, polisi hawawezi kuendelea kukusanya uchunguzi wa tukio?



Columnist: mwananchi.co.tz