Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Tunahitaji udhibiti wa vitabu vya kitaaluma

13106 Pioc+vitabu TanzaniaWeb

Tue, 21 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Chuo Kikuu cha Manchester kinatoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi kutoka katika nchi mbalimbali za Afrika wanaotaka kujiunga chuoni hapo.

Ufadhili huu ni wa ngazi ya shahada ya pili katika kozi za Uhandisi,mazingira, sheria, sayansi ya maisha na elimu.

Jumla ya nafasi 27 zimetengwa kwa ajili ya ufadhili kwa ajili ya wanafunzi kutoka Afrika Tanzania ikiwemo.

Watakaofanikiwa kupata ufadhili huu watalipiwa nauli za ndege, gharama za viza, ada na gharama zote za maisha kwa mwanafunzi anapokuwa chuoni.

Vigezo

Mwombaji anatakiwa afahamu ni kwa namna gani ufadhili huo utamsadia yeye binafsi na jamii yake

Mwombaji anatakiwa awe amepata daraja la kwanza la ufaulu katika shahada yake ya kwanza

Mwombaji anatakiwa awe na uzoefu wa kufanya kazi kwa muda usiopungua miaka miwili

Mwisho wa maombi: Septemba 9, 2018

Tuma maombi: https://scholarship-positions.com

Chuo Kikuu cha Sheffield Hallam kinatoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa mataifa yanayoendelea wanaotaka kujiendeleza kielimu.

Ufadhili huu ni kwa wanaotaka kujiunga na shahada ya kwanza na shahada ya uzamili kwa mwaka wa masomo 2019.

Ufadhili huu utatolewa chuoni Sheffield Hallam ambacho kipo nchini Uingereza

Vigezo

Mwombaji anatakiwa awe amefaulu kwa kiwango cha juu

Kwa wanafunzi wa shahada ya kwanza wanatakiwa kuwasilisha vyeti vinavyoonyeshau ufaulu katika somo la kiingereza

Mwisho wa maombi: Novemba 1, 2018

Tuma maombi: www.shu.ac.uk/transformtogether

Taasisi ya wanawake wa Afrika inatoa fursa kwa wanawake kutoka bara la Afrika kushiriki kwenye mafunzo yatakayofanyika nchini Hispania.

Mafunzo haya yanalenga kumjengea uwezo mwanamke wa Afrika na kumuwezesha kushiriki katika masuala mbalimbali kwenye jamii.

Mafunzo hayo yatahusisha ufanyaji wa tafiti katika maeneo mbalimbali yanayogusa maisha ya kila siku ya mwanadamu.

Maeneo yatakayofanyiwa utafiti ni pamoja na afya, nishati, maji na mabadiliko ya tabia nchi, kilimo na usalama wa chakula na kozi nyingine kadhaa.

Mwisho wa maombi: Septemba 30, 2018

Tuma maombi: https://www.mujeresporafrica.es

Mfuko wa ufadhili wa Rhodes unatoa fursa za ufadhili kwa wanafunzi wanaotaka kujiendeleza kielimu katika chuo kikuu cha Oxford cha Uingereza.

Ufadhili huu uko wazi kwa mtu yeyote kutoka taifa linaloendelea mwenye nia ya kuongeza umahiri wake katika elimu

Vigezo

Mwombaji lazima awe ametoka taifa linaloendelea

Athibitishe kuwa hana uwezo wa kujigharamia masomo. Mwombaji anatakiwa awe na shahada ya kwanza kwenye kozi anayoombea ufadhili

Mwombaji pia anatakiwa awe ameandaa nyaraka zinazoelezea utafiti atakaofanya

Umri wa mwombaji hautakiwi kuzidi miaka 28. Mwisho: Oktoba 2018

Tuma maombi: http://www.rhodeshouse.ox.ac.uk/

Imeandaliwa na Elizabeth Edward

Columnist: mwananchi.co.tz