NCHI za Afrika hasa Kusini mwa Jangwa la sahara zimeshauriwa kuwa zikitaka kuvuna faida za maendeleo ya teknolojia ya kidijitali lazima ziwekeze kwa watoto na kuhakikisha wanapata elimu ya kidijitali ili kukuza ujuzi wao.
Ushauri huo upo katika repoti za Benki ya Dunia ambapo imesema maendeleo haya ili yawe na faida zaidi siku zijazo imeshauriwa wananchi wapewe elimu hata ya msingi ya kidijitali, ilitaja baadhi ya elimu ili kuweza kutumia mawasiliano ya barua pepe, kufanya tafiti kwa kutumia mtandao, malipo mtandaoni, kutunza data kwa kutumia programu maalumu za Kompyuta.
Baadhi ya kampuni za simu nchini, hivi karibuni zilianza kutekeleza ushauri huo, kwa kuanza kuwekeza kwa wanafunzi ili kukuza ubora wa nguvu kazi ya kizazi kijacho.
Mfano Kampuni Tigo Tanzania mwaka 2019 ilizindua kampeni ya kuelimisha wanafunzi wa kike ujuzi wa namna mbalimbali kama uandishi wa programu za kompyuta (coding) na uchambuzi wa taarifa, ushauri huo ulisisitiza kampuni zingine kuiga mfano wa Tigo Tanzania.
Hata hiyvyo, Teknolojia ya Kidigitali inavokuwa kwa kasi kwa upande wa mawasiliano hasa simu za mkononi imesaidia kwa kiasi kikubwa kukua na kuendelea kiuchumi kwa nchi nyingi za Afrika hasa Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Pia imeelezwa Kukua kwa uchumi na kuendelea kwa kasi eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara kumesababishwa na kuongezeka kwa matumizi ya simu za mkononi na matumizi ya mtandao 'intaneti'.
Pia Soma
- Majaliwa: Mtumishi asiyefuata maadili hatufai
- VIDEO: Ubalozi wa China watoa neno kuhusu wanafunzi waliopo Wuhan
- Ujumbe wa Maalim Seif kwa Magufuli
Takwimu hizo, zinaonesha mbali na ajira pia kuna fursa zingine ambazo vinapatikana na kuzitaja fursa hizo kuwa ni eneo la Kilimo kwani teknolojia hiyo inabadilisha mambo kuwa bora na kisasa zaidi, baadhi ya wakulima katika nchi za Ethiopia, Kenya na Rwanda sasa wanapata taarifa za soko la mazao, hali ya hewa na hata nini cha kupanda kwenye udongo wa namna gani, kupitia simu zao za mkononi.
Takwimu hizo, zimeonesha mabadiliko haya yanaongeza tija kwenye kilimo na kwa ujumla kwani yanabadili maisha ya watu kuwa bora, kisasa na rahisi.
Taarifa za Benki ya Dunia zimetoa mfano kuwa fursa katika sekta ya mawasiliano zimesaidia kukuza uchumi wa mamilioni ya watu kwani teknolojia ndiyo inaendesha biashara, wafanyabiashara wengi wanaweza kuagiza malighafi na kupokea malipo toka kwa wateja kirahisi.