Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Tazama matukio katika picha kutoka Bungeni leo – June 1, 2018

8558 1 3 TZW

Sun, 3 Jun 2018 Chanzo: bongo5.com

Kikao cha 42, mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeendelea Jijini Dodoma, Leo Bunge limeongozwa Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson. Kipindi cha Maswali na Majibu kiliendelea na wabunge walijibiwa na Serikali.



Waziri wa Katiba na Sheria,Palamagamba Kabudi akizungumzia umuhimu wa kutunza rasilimali za Taifa kwa maslahi ya kizazi hiki na kijacho wakati akichangia mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Madini kwa mwaka 2018/2019 leo Bungeni Mjini Dodoma



Mbunge wa Muheza, Balozi Adadi Rajabu akizungumzia mchango wa sekta ya madini wakati wa mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Fedha ya Wizara ya Madini leo Bungeni Jijini Dodoma

Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Singida,Martha Mlata akizungumzia umuhimu wa hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kulinda rasilimali madini wakati wa mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Madini kwa mwaka 2018/ 2019



Waziri wa Madini,Angellah Kairuki akitoa hotuba ya kufunga maonesho ya madini yaliyofanyika kwa siku mbili katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma



Mjiolojia Mwandamizi kutoka Wakala wa Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST) Bw. Octavian Minja akisisitiza jambo kwa mmoja wa wananchi waliotembelea maonesho ya Madini yaliyofanyika katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma



Sehemu ya washiriki wa maonesho ya madini yaliyofanyika katika viwanja vya Bunge wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Madini wakati akifunga maonesho hayo leo Jijini Dodoma



Mmoja wa washiriki wa maonesho ya madini yaliyofanyika katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma Bi Susie Kennedy akifurahia jambo na Waziri wa Madini wakati akikabidhiwa cheti cha ushiriki wakati wa hafla yakufunga maonesho hayo leo Jijini Dodoma

Sehemu ya wageni waliofika Bungeni wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu Bungeni Jijini Dodoma leo



Sehemu ya mabanda ya maonesho ya Madini kama inavyoonekana katika picha ndani ya Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma

Loading...
Columnist: bongo5.com