Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Tatizo letu ni kubwa kuliko tunavyofikiria

64544 Tatizo+pic

Thu, 27 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mtu makini anaweza kutambua kwamba tatizo letu ni kubwa zaidi ya tunavyofikiri. Hili ni tatizo la Watanzania wote. Si la CCM wala vyama vya upinzani bali letu sote.

Sina lengo kuwatetea wanasiasa, bali nataka kuwa mbali na ushabiki ili tushirikiane sote kubaini tatizo letu; nini kimetufikisha hapa; kwa nini tunakubali kutawaliwa na fedha badala ya busara, hekima, uadilifu, uzalendo na ujuzi wa mambo?

Siku za hivi karibuni nilikutana na watu watatu tofauti. Tofauti zao si za maumbile wala sura, bali maoni. Bahati nzuri nilikutana nao kwa nyakati tofauti, la wangetoana macho au roho, maana walikuwa wanatumia hoja ya nguvu.

Mtu wa kwanza alikuwa mpinzani wa CCM – kwa maoni yake, CCM ni chukua chako mapema, ni chama cha rushwa au ufisadi. Aliamini kwamba uozo wote nchini ni kazi ya CCM – rushwa, kutowajibika, ukabila na udini, majanga, na hata Ukimwi ni kazi ya CCM.

Mtu huyu aliongezea kwamba CCM imeharibu uchumi na kuwaathiri Watanzania wote kiakili na kiutendaji. Alikuwa na hasira ya kutisha; hasira iliyo ndani ya mioyo ya baadhi ya Watanzania.

Mtu wa pili ni mwana CCM. Alikuwa hana hata kandambili, alivaa matambara; aliniomba Sh2,000 kumpeleka mtoto hospitali. Alikuwa anaisifia CCM kwa nguvu zake zote.

Pia Soma

Alisema CCM ni chama cha kuleta maendeleo, chama cha watu na ndicho chama cha mapinduzi ya kweli. Ukiisoma ilani ya uchaguzi ya CCM, utakubaliana naye kwamba ana haki zote za kusifia chama hicho. Ilani ni nzuri sana, utekelezaji ndiyo tatizo.

Mtu wa tatu niliyekutana naye ni mwanamageuzi. Huyu kama yule wa kwanza haipendi CCM. Imani yake ni kwamba ili nchi hii ifikie mapinduzi ya kweli, ni lazima itawaliwe na chama cha upinzani. Ushawishi wa mtu huyu ulikuwa mzito kiasi cha kukubaliana naye aliyokuwa akiyasema yote ni kweli.

Rafiki yangu mmoja ni fundi stadi wa kushona suti, za kike na kiume. Ana wateja wengi na familia yake inaishi kwa kipato hicho. Yakiingia makambi ya maombi na miujiza ya uponyaji, rafiki yangu huyu anafunga kazi zaidi ya mwezi mzima.

Hapo hakuna tena cha wateja wala familia. Anashinda na kulala kwenye maombi mwezi mzima hadi miwili na wakati mwingine anazunguka na vikundi hivi vya maombi kwa kipindi cha miezi sita. Wateja wake wanaikosa huduma ya kushonewa suti na familia yake inakosa matunzo, maana kipato kinapungua kwa vile anakuwa hafanyi tena kazi ya kuzalisha.

Rafiki yangu mwingine amepoteza watoto watatu kwa kutokuwa na imani na dawa za hospitali. Yeye anaamini katika sala na miujiza ya uponyaji. Miujiza haiwezi kutibu malaria, ni lazima kunywa dawa vinginevyo mtu anakufa.

Lengo la makala hii ni kuonyesha kwamba si kila uozo unasababishwa na CCM na si kweli kwamba tukibadilisha chama nchi yetu itajaa neema tele.

Tunaweza kubadilisha chama, lakini watu wakabaki ni walewale: Watu wasiokubali mabadiliko, wasiotafuta ukombozi wala mapinduzi ya kweli.

Ukombozi wa fikra ndicho kitu cha msingi kwa kipindi hiki tulichomo.

Kila mtu anahusika na maendeleo ya nchi yetu. Tukimbilie kujisahihisha, kujibadilisha na kujisafisha wenyewe, kila mtu kwa nafasi yake na kila mtu binafsi.

Columnist: mwananchi.co.tz