Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

TUONGEE KIUME: Ukweli wasioujua mabinti zetu kuhusu kuolewa

97582 Kuolewa+pic TUONGEE KIUME: Ukweli wasioujua mabinti zetu kuhusu kuolewa

Mon, 2 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tuifufue hii hadithi... Mwanaume mmoja alikwenda kuomba ushauri kwa mzee mwenye hekima. Akamuuliza, ‘Babu, nina wanawake watatu, nataka kuoa mmoja, nioe yupi?’

Babu akamwambia nenda kwa wanawake wote watatu, wagawie kiasi sawa cha pesa kila mmoja. Kisha kati yao, atakayetumia kwenye mambo ya msingi ya kukusaidia wewe, yeye na kesho yenu huyo ndiye ana sifa ya kuwa mkeo.

Ikawa hivyo, akawagawia wanawake wote watatu kiasi sawa cha pesa.

Wa kwanza akaenda saluni, akaweka nywele mpya, kope mpya, kucha mpya, akanunua nguo mpya, manukato mapya na makokoro kibao ya urembo. Hela yote ikaishia huko. Akarudi kwa mwanaume kumuonyesha jinsi alivyopendeza.

Wa pili akaenda saluni pia, akajitia mazagazaga yote ya urembo, akapendeza kumkaribia yule wa kwanza, lakini yeye hakutumia pesa yote. Iliyobaki akaenda kumnunulia mwanaume shati jipya na kumpelekea kama zawadi.

Watatu hakuichukua ile pesa, ila akamwambia mwanaume, ‘mpenzi, hii pesa ni nyingi inatosha kuwa mtaji wa biashara yenye kueleweka kabisa.’ Akataka wafungue biashara. Ikawa hivyo kwa msaada wa mwanamke ile pesa ikatumika kufungulia biashara ambayo baada ya muda ikaanza kuingiza faida na wakapata zaidi walichokuwa nacho.

Pia Soma

Advertisement
Basi mpaka hapo ilikuwa wazi kuwa mwanamke aliyestahili kuwa mke kwa mujibu wa ushauri wa babu ni huyu wa tatu.

Basi mwanaume naye wala hakufanya ajizi kuchagua wa kumuoa.

Kwa nini nimetaka tuirudie hii hadithi? Kwa sababu mijini siku hizi moto umewaka. Wadada wanatafuta ndoa kwa kasi na mbinu zote kama mwanasiasa anayependa faida za kupigiwa kura lakini hapendwi na wapiga kura.

Wanawake wanatumia kila namna kupata ndoa. KIpaumbele kwao ni moja kuolewa, mbili kuolewa na tatu kuolewa.

Lakini kama ndoa ni jambo jema kwa nini ipiganiwe sana na upande mmoja? Swali hili likaniletea jibu kwamba wanawake wanatafuta sana ndoa kwa sababu wengi wao hawana malengo yoyote.

Wakitazama kesho wanachokiona ni kuolewa, kupata watoto, kisha wajukuu, kuzeeka halafu kufariki. Kwa hiyo ukiitoa ndoa kesho yao inakuwa ni kuzeeka na kufa hawataki.

Wakati vijana wengi wa kiume wenyewe wakitazama kesho, wanaona wanamiliki biashara kubwa, kampuni, wanavumbua vitu vikubwa vya kuisaidia jamii na miradi mikubwa. Kwa hiyo hata ukichomoa ndoa bado wana sababu nyingine za kuendelea kuishi.

Sote hapa tuna mabinti, watoto wa kike, dada zetu hivyo ni bora tuwaeleze ukweli wa maisha. Ndoa ni suala la bahati tu, halihitaji maandalizi ya kiasi kikubwa kama wanavyoamini. Anaweza mtu akakudanganya kama unataka kuolewa kuwa hivi, ukawa hivyo na ukazeeka bila ndoa. Hakuna tatizo kama utakuwa mwanamke unayejielewa, unamiliki biashara au kuongoza kampuni kubwa bila kuolewa, na ukiwa na sifa hizo bila shaka utaolewa hakuna anayetaka kuoa mwanamke anayefikiria mwisho wa vidole vya miguu yake, wanataka anayeona mbali.

Kwa hiyo ni vyema kabla hawajawaza ndoa, waweke malengo binafsi ya maisha yao ambayo hayategemei ndoa kwani huwa inakuja yenyewe bila kulazimishwa kwa kujibadili, kujiremba wala kujidhalilisha kwa waganga na nyumba za ibada.

Hatusemi kwamba kuolewa ni jambo baya, hapana. Tunachosema ni dunia haijawahi kumkumbuka mwanamke kwa sababu ameolewa, inawakumbuka wanawake waliokuwa na malengo ya kufanya mambo makubwa na kutimiza malengo yao. Usikubali kuchanganywa na siasa za ndoa.

Columnist: mwananchi.co.tz