Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

TFF sasa inapoteza mwelekeo na hii fungiafungia yake

33201 Ibra+Bakari Tanzania Web Photo

Mon, 24 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Miaka ya nyuma, linapofika pambano la watani, Simba na Yanga suala la wachezaji kurusha njiwa lilikuwa jambo la kawaida.

Pamoja na kwamba ilisemekana ni mambo ya kishirikisha, lakini ilinogesha pambano. Njiwa anapoachiwa huenda kutua kwenye goli na hapo mashabiki huamini kuwa mabao yatamiminika hapo.

Hilo huamsha kelele za mashabiki na timu inayoanza lango ambalo njiwa hutua, basi hofu hujaa tele.

Lakini ilikuwa ni tofauti kabisa, ile ni kama kufurahisha umati kwani timu zilirusha njiwa lakini zikafungwa kama kawaida.

Nimeanza na hiyo ya mahasimu kama kibwagizo tu, lakini kubwa ni kutaka kuegemea kwenye hili ambalo limenisukuma kuandika haya. Suala la Ibrahim Job na Hassan Dilunga kufungiwa mechi tatu na faini juu.

Novemba 23, 2018 Simba ilicheza na Lipuli mechi ya Ligi Kuu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam iliyomalizika kwa suluhu.

Katika mchezo huo, kiungo wa Simba, Dilunga na beki wa Lipuli FC Ibrahim Job wamefungiwa michezo mitatu na kupigwa faini ya Sh500,000 kila mmoja.

Kilichoelezwa kuwa ni kutokana na eti kukiuka sheria za kutokuingia vyumbani wakati timu zikienda mapumziko. Dilunga pamoja na Ibrahim walisalia dimbani wakati wenzao wakiwa vyumbani baada ya kumalizika kipindi cha kwanza.

Kilichotokea ni kwamba ilikuwa kama kufurahisha umati kwani kutoka au kutotoka uwanjani hakuna uhusiano wowote na mechi kwani kama kutoka uwanjani walitoka na kwenda vyumbani.

Kinachonishangaza ni hiyo kufungiwa na kutozwa faini. Kama kuchelewa kuingia vyumbani, nikajiuliza kama ingekuwa wamegongana na kuendelea kugangwa, na mpira ukaingia mapumziko navyo wangefungiwa kwa sababu wameumia?

Kama ingekuwa kiatu kimevuka, mchezaji akawa anavaa na mpira ukaingia mapumziko, nayo angesimamishwa? Nilisikitikia hatua hiyo baada ya kumsikia kocha wa Lipuli, Selemani Matola akilalamikia hali hiyo, huku akilalamikia TFF ndiyo waamuzi wa kufanya wanachotaka.

Ukweli hii inavunja nguvu na haina maana kwa kuwa klabu hazina fedha na TFF inazikandamiza kwa njia hii.



Columnist: mwananchi.co.tz