Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Super Sunday Makala: Je, Teknolojia ni Laana au Baraka katika afya zetu?

8593 Shutterstock 135034070 TZW

Mon, 4 Jun 2018 Chanzo: bongo5.com

/>

Vifaa vya kisasa vimebadili njia za kufanya mambo na vimerahisisha kazi nyingi ngumu, taaluma za kitiba zimepiga hatua kubwa katika kupigana na magonjwa, hivyo kuboresha afya za wengi, hata hivyo hilo limetuleta madhara mengi.

Mkurugenzi Mkuu wa Impact Afya, Bhakti Shah anasema ingawa teknolojia ya kisasa imeboresha afya lakini kadiri muda unavyopita imefanya watu wengi kukaa bila kufanya mazoezi ya kutosha.

Katika ripoti iliyochapishwa hivi karibuni yenye kichwa ‘International cardiovascular diseases statistics, Shirika la Moyo la Marekani lilieleza kuwa mabadiliko ya kiuchumi, watu kuhamia mijini, ustawi wa viwanda na kuenea kwa biashara za kimataifa, huleta mabadiliko katika mitindo ya maisha ambayo huchangia ugonjwa wa moyo.

Ripoti hiyo inataja kutofanya mazoezi na kula vyakula visivyofaa kunachangia sana ugonjwa huo. Mtindo wa maisha wa leo wa mijini umechangia kiasi kikubwa kuwa na ongezeko la madhara yatokanayo na kutofanya mazoezi.

Mfanyakazi anaweza kuketi ofisi siku nzima bila kwenda sehemu yoyote, kisha jioni kuchukua gari lake na kwenda nyumbani kupumzika.

Nchini Marekani ambako asilimia 25 ya safari zote hazizidi kilometa moja, inaelezwa asilimia 75 ya safari hizo fupi kufanywa kwa gari.

Teknolojia ya kisasa imefanya watoto wakae tu bila kufanya mazoezi ya kutosha, uchuguzi mmoja ulionesha kwamba kadiri michezo ya video inavyozidi kuwa yenye kufurahisha na halisi, ndivyo watoto wanavyotumia wakati mwingi zaidi kuicheza.



Mikandaa kama hiyo imefikiwa kuhusu kutazama televisheni na vitumbuizo vingine ambavyo huwafanya watoto wakae tu bila kufanya mazoezi ya kutosha.

Hatari Yake

Shah anasema watoto wasiofanya mazoezi wanaweza kukabiliwa na hatari ya kutojiheshimu, kuwa na wasiwasi mwingi na mafadhaiko mengi, kuna uwezekano mkubwa watoto hawa wakaja kuvuta sigara na kutumia dawa za kulevya.

“Wafanyakazi wasiofanya mazoezi hukosa kwenda kazini mara nyingi kuliko wale wanaofanya mazoezi,” anasema.

“Wanapozeeka watu wasiofanya mazoezi hupoteza nguvu kuliko wale wanaofanya mazoezi, matokeo ni kwamba wengi hushindwa kujitegemea na afya zao za akili kuzorota,” anasisitiza.

Rais wa taasisi ya utafiti wa mazoezi na mtindo wa maisha ya Canada, Cora Craig anaeleza kwamba Wakanada wengi hawafanyi kazi ngumu kama hapo awali, kwa ujumla ni wachache wanaofanya kazi hizo.

Gazeti la kanada Globe and Mail liliripoti kuwa asilimia 48 ya Wakanada ni wazito kupita kiasi, wakati asilimia 15 ni wanene kupita kiasi. Pia gazeti hilo linaongeza kwamba asilimia 59 ya watu wazima hawafanyi mazoezi.

Dkt. Matti Uusipa wa Chuo Kikuu cha Kuopio, Finland anaonya kwamba wagonjwa wa kisukari ambao kwa kawaida huwapata watu wazima unaongezeka kwa haraka ulimwenguni kwa sababu watu wengi wamekuwa wanane kupia kiasi na hawafanyi mazoezi.

Nchini Hong Kong uchunguzi ulionesha kwamba huenda asilimia 20 ya vifo vyote vilitokea miongoni mwa watu walio na umri wa miaka 35 au zaidi vilisababishwa na kutofanya mazoezi.

Uchuguzi huo ulioongozwa na Prof. Tai Hing Lam wa Chuo Kikuu cha Hong Kong na kuchapishwa na jarida la Annals of pidemiology mwaka 2004.

Utafiti huo ulimalizia kwa kusema kwamba kwa Wachina wanaishi Hong Kong ‘hatari za kutofanya mazoezi zinapita zile za kutumia tumbaku’, watafiti wanatabiri kwamba raia wengi wa China watapatwa na madhara hayo hayo.

Tanzania Inapaswa Kuogopa?

Na je ni kweli kutofanya mazoezi kunaweza kudhuru afya zetu kuliko kuvuta tumbaku, na kama ni hivyo nani wa kulaumiwa?.

Shah anasema watu wengi wasiofanya mazoezi huelekea hatari kubwa ya kupatwa na kiharusi, ugonjwa wa moyo, aina flani ya kansa, ugonjwa wa mifupa, na uwezekano mkubwa wa kuwa mnene kupita kiasi ukilinganishwa na watu wanaofanya mazoezi.

Gazeti la Wall Street Journal linaripoti kuwa katika kila bara ulimwenguni idadi ya watu wazito au wanene kupita kiasi inaongezeka kwa kasi sana.



Ripoti hiyo ilisema tatizo hilo linasababishwa hasa na kula vyakula vyenye karoli nyingi na kutofanya mazoezi, kinadharia ni magonjwa zaidi ya 23 yanayotokana na kutofanya mazoezi.

Watu wengi ulimwenguni hawafanyi mazoezi yoyote na inavyostahili. Shirika la moyo ulimwenguni linaamini kwamba kati ya asilimia 60 hadi 85 ya watu ulimwenguni hasa wasichana na wanawake hawafanyi mazoezi ya kutosha ili kupata manufaa ya afya.

Shirika hilo linadai kwamba karibu heluthi mbili ya watoto pia hawafanyi mazoezi, karibu nusu ya vijana wenye umri wa kati ya miaka 12 na 21 hawafanyi mazoezi magumu kwa kwaida.

Shirika la afya ulimwenguni (WHO) linaripoti kwamba kila mwaka watu milioni mbili hufariki ulimwenguni kwa kutofanya mazoezi.

Shah anasema ili kukabili halo mashirika ya kiserikali ulimwenguni yamezisha kampeni za kuelimisha umma kuhusu manufaa ya kufanya mazoezi kwa kiasi. Kufikia mwaka 2020, Australia, Japan na Marekani zinamatumaini kuwa idadi ya wanaofanya mazoezi itaongezeka kwa asilimia 10.

WHO inaeleza nchi nyingine zilizojiunga katika hii kampeni ni pamoja na Mexico, Brazili, Jamaika, New Zealand, Finland, Urusi, Morocco, Afrika Kusini, Vietnam, na Slovenia.

Watoto na Mazoezi

Uchuguzi wa hivi karibuni umegundua kwamba watoto wengi hawafanyi mazoezi hasa watoto wa kike kuliko wa kiume, inaonekana kadri watoto wanavyokuwa hupunguza kiasi cha kufanya mazoezi.

Shah anaeleza kufanya mazoezi kwa watoto husaidia kuwa na mifupa na misuli yenye nguvu na viungo vyenye afya, kuzuia uzito na unene kupita kiasi.

“Pia huondoa uwezekano wa kupatwa na shinikizo kubwa la damu, kujiheshimu zaidi, kuzuia wasiwasi na kupata mfadhaiko,” anasema.

Vipi Kuhusu Wazee?

Inaelezwa kadiri wanavyozeeka ndivyo unavyoweza kunufaika kwa kufanya mazoezi kwa kiasi, hata hivyo wazee wengi husita kufanya mazoezi kwa ukawaida kwa kuogopa kwamba wataumia au watakuwa wagojwa.



“Ni kweli wazee wanapaswa kutafuta ushauri wa daktari kabla ya kuanza kufanya mazoezi magumu,“ anasema Shah.

Wataalamu wanaamini kwamba kufanya mazoezi kunaweza kuboresha maisha ya wazee na kuna faida zake pia. Faida hizo ni kama kuwa chonjo kiakili, usawaziko na unyumbuliko, afya ya kihisia, kupona haraka ugonjwa au jereha na kuboresha utendaji wa tumbo.

Dondoo Muhimu

Kulingana naShirika la Moyo la Marekani, kutofanya mazoezi huongeza maradufu hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo na kuzidisha kwa asilimia 30 hatari ya kupata shinikizo kubwa la damu, pia uongeza maradufu uwezekano wa kufa.

Nchi ya Australia hutumia dola milioni 377 kila mwaka kutibu matatizo yanayosababishwa na kutofanya mazoezi.

Kwa mujibu wa shirika la moyo ulimwenguni, nchi ya Canada kila mwaka hutumia zaidi dola bilioni mbili kutibu matatizo ya afya, wakati mwaka 2000 nchi ya Marekani ilitumia dola bilioni 76.

Loading...
Columnist: bongo5.com