Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Siri ya ziara ya mwanamapinduzi Che Guevara nchini Tanzania

53241 Pic+cehgavara

Sat, 20 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanamapinduzi wa Argentina na shujaa wa mapinduzi ya Cuba, Ernesto “Che” Guevara, alitumia zaidi ya miezi minne nchini Tanzania kati ya 1965 na 1966.

Aliingia katika ardhi ya Tanzania mara tatu, mara moja kwa wazi na mara mbili kwa siri kati ya Februari na Novemba ya 1965.

Che alivutiwa na Tanzania kwa sababu ilikuwa makao makuu ya harakati nyingi za ukombozi kusini mwa Afrika; ilikuwa ni moja ya vituo vya mageuzi ya mapinduzi katika bara la Afrika wakati huo.

Baada ya karibu miezi mitatu ya kusafiri kwenda nchi sita za Afrika kuongeza mwamko kwa ajili ya mapinduzi, Tanzania ndiyo Serikali yake ilikuwa tayari kusaidia mpango wake Che na kumkaribisha kwa ajili ya kuzindua mapinduzi yake.

Tanzania hatimaye itakawa hatua ya kwanza ya kuanza kwa operesheni ya Cuba ambayo ingeweza kuona Che pamoja na zaidi ya Wacuba 130 wakivuka Ziwa Tanganyika na kutumia miezi saba kupigana huko Congo.

Che alitua Dar es Salaam Alhamisi ya Februari 11, 1965 akitokea China. Alikuwa na mkakati mmoja: kuunganisha harakati za ukombozi na kuunda jeshi la umoja kupigana dhidi ya mabeberu na ukoloni mambo leo nchini Congo.

Che alikuja Tanzania akiwa na mkakati wa aina hiyo. Alitaka mapinduzi. Kama kulikuwa mahali ambako ungeweza kukutana na idadi kubwa ya wapigania uhuru na wanamapinduzi kutoka mataifa mbalimbali waliokusanyika katika nchi moja, basi sehemu hiyo ilikuwa Tanzania katika kipindi cha mwaka 1965.

Vita lilikuwa ikipamba moto katika taifa jirani la Msumbiji dhidi ya Wareno. Wapigania uhuru kutoka Afrika Kusini, Zimbabwe, na Namibia, walikuwa wakiingia ndani ya Tanzania.

Hivyo, Tanzania ilikuwa sehemu moja ya Afrika ambayo Che alikuwa na matumaini ya lengo lake la kuajiri wapiganaji na kuanzisha msingi wa vita kwa mapinduzi.

Che alitumia siku ya kwanza Dar es Salaam na kisha akaruka kwenda Zanzibar kuhudhuria maadhimisho ya kumbukumbu ya maadhimisho ya mapinduzi ya Zanzibar mwishoni mwa wiki ya Februari 13, 1965.

Mkutano huo uliahirishwa kuanzia Januari 12 hadi Februari 12, 1965 kwa sababu ya Ramadhan. Kuhudhuria maadhimisho hayo ilikuwa mwanzo wa mfano wa ziara ya Che ya Tanzania. Cuba ilitoa mafunzo ya kijeshi kwa marafiki wengi wa Zanzibar ambao walikuja kuchukua jukumu kubwa katika ushindi wa mwisho wa mapinduzi hayo.

Hali ya usalama nchini Tanzania mwishoni mwa mwaka wa 1964 na mwanzoni mwa 1965 ilikuwa tete. Mgogoro wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Marekani ulikuwa umeanza Novemba 1964 na kupatikana kwa nyaraka zinazoelezea mpango na Marekani kusaidia Ureno kuiangusha Serikali ya Tanzania.

Mgogoro huo uliongezeka zaidi Januari 11, 1965, wakati maofisa usalama wa Tanzania waliponasa mazungumzo ya simu ya wanadiplomasia wawili wa Marekani, Bob Gordon na Frank Carlucci, waliosikika wakizungumza kwa namba kuhusu kile kilichoonekana kuwa njama dhidi ya Serikali ya Zanzibar.

Wanadiplomasia hao wa Marekani walifukuzwa kutoka Tanzania Januari 1965. Che alikuwa Tanzania wakati huo. Februari 15, 1965, The New York Times lilichapisha habari juu ya mgogoro wa kidiplomasia kati ya Marekani na Tanzania likibainisha kuwa Serikali ya Tanzania ilikuwa ikimhifadhi Che Guevara wakati wa mgogoro huo.

Huko Zanzibar, Waziri wa Elimu, Ali Sultan Issa aliyekuwa ameteuliwa karibuni alipewa jukumu la kumhifadhi Che. Ali alikuwa mjamaa ambaye alikuwa amesoma Uingereza baadaye alitumia muda wake kukaa huko Cuba na China. Ali alikutana naye kwa mara ya kwanza Cuba mwaka 1962 na tena baada ya walikutana kwenye kongamano moja lililofanyika Geneva, Uswisi mwaka 1964. Che alikaa katika kijumba kidogo huko Buba, Zanzibar, chini ya maandalizi ya Ali.

Wawili hao walitumia saa mbili kujadili maono ya Che kuhusu harakati hizo. Che alitaka kujenga majeshi ya mapinduzi kutoka kwa mabara matatu tofauti, Afrika, Amerika ya Kusini na Asia kupigana dhidi ya madola ya magharibi. Wawili hao pia walijadili kuamka kwa mawazo ya mapinduzi ya Afrika kati ya waasi nchini Congo, wapigania uhuru nchini Msumbiji na kusini mwa Afrika.

Che alikutana na Dk Salim Ahmed Salim na familia yake Zanzibar. Dk Salim alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Misri tangu 1964 hadi 1965. Alimwalika Che nyumbani kwake kwa chakula. Alirudi Dar es Salaam baada ya kutumia siku kadhaa Zanzibar.

Mipango ilifanyika kwa mkutano kati ya Che na wawakilishi angalau asilimia 50 ya makundi ya kupigania uhuru kutoka nchi 10. Balozi mweusi wa Cuba nchini Tanzania, Pablo Rivalta na Mkuu wa Amerika ya Kusini, Idara ya Upelelezi kwa Cuba, Juan Carretero walihusika katika mazungumzo hayo. Mkutano ulifanyika katika Ubalozi wa Cuba Upanga, Dar es Salaam.

Professor Azaria Mbughuni

Lane College, USA

[email protected]

Twitter @AzariaTZ

Makala hii ambayo kwa mara ya kwanza imechapishwa na gazeti la The Citizen itaendelea kesho.



Columnist: mwananchi.co.tz