Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Shemeji zangu wakali kuliko mke wangu, wananitoa udenda

Shemeji zangu wakali kuliko mke wangu, wananitoa udenda

Tue, 5 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Anti habari!

Samahani kwa hili nilisemalo, napata wakati mgumu mke wangu analeta ndugu zake wakali kuliko yeye na wana mitego kiasi kwamba ninaingia majaribuni.

Nifanyeje?

Acha tamaa, umeziendekeza ndiyo maana zinakupelekea puta.

Kama mkeo ni mwelewa mwambie kinagaubaga kuhusu tatizo lako dhidi ya hao ndugu zake, akiwa na nia ya kunusuru ndoa yake atakusikia. Lakini akiichukulia kwa mtizamo hasi hiyo kauli yako utazua utata mpya.

Ukishindwa kumueleza kuwa unapata matamanio awaondoe mweleze wabadili aina za mavazi kwa sababu hayana maadili, labda wakijistiri kidogo itasaidia kuondoa tatizo ulilonalo.

Ila muombe sana Mungu akuondolee jinamizi baya ulilonalo. Hivi ukijua tu huyu ni shemeji yako si inatosha kuwa na nidhamu unapomuona.

Mthamini mkeo, kuwaona wadogo zake wakali kuliko yeye ni kumdharau.

Kwa ‘samba’ hili nitashindwa

Nimeolewa huu mwaka wa nne, najisifu si haba samba nalicheza na ninalijua, lakini mwenzangu hatosheki kiasi naelekea kushindwa.

Nifanyeje?

Umesema samba unaliweza mbona unalalamika kushindwa tena?

Pambana usikubali kushindwa, huu mchezo hauna kuacha ni kuongeza manjonjo.

Fanya hivi ili asikuchoshe. Kwa sababu samba unalijua tumia nafasi hiyo kumchosha mapema kwa kumshika maeneo unayoamini ukiyashika hapindui lazima akubali muziki wako fasta.

Anaweza kukukataza. Jitoe fahamu na ujifanye kama hujamshika maeneo hayo hupati kile mlichokusudia, akikuuliza mchezo huo umeanza lini...Mwambie kwa kujiamini umeanza leo (Kwa sauti ya utulivu na ulimi uliolainika).

Usiniangushe, mwanajeshi hodari huwa wa mwisho kusalimu amri.



Columnist: mwananchi.co.tz