Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Sauti ya Rais Reagan yavuja Akiwaita Watanzania tumbili

69319 Tumbili+pi

Thu, 1 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Washington, Marekani. Rais wa zamani wa Marekani, Ronald Reagan anatumiwa kuwaita tumbili wajumbe wa Afrika katika Umoja wa Mataifa UN mwaka 1971 wakati alipokuwa gavana wa Jimbo la California katika ukanda wa sauti uliochapishwa na The Atlantic.

Sauti hiyo ilifichuliwa jana na Profesa wa Historia katika Chuo Kikuu cha New York, Tim Naftali ambaye alikuwa mwelekezi katika maktaba ya Rais Nixon.

Maktaba hiyo ilihifadhi kanda zote zilizorekodiwa za Rais huyo kutoka mwaka 2007 hadi 2011.

Inadaiwa kuwa Reagan ambaye kipindi hicho alikuwa gavana alitoa matamshi hayo ya kibaguzi katika mawasiliano yake ya simu kwa aliyekuwa Rais wa Marekani Richard Nixon ambaye alirekodi simu zake zote

Gavana huyo alikasirishwa na hatua ya wajumbe wa Afrika katika Umoja wa Mataifa (UN) kutounga mkono Marekani katika kura ya kuitambua China na kuipiga marufuku Taiwan. Inadaiwa kuwa baada ya kura hiyo, wajumbe wa Tanzania walikuwa wameanza kucheza densi katika ukumbi wa UN.

Inaelezwa kuwa wakati Reagan alipompigia simu Rais Nixon siku iliofuata alimuuliza iwapo alikuwa ameshuhudia kura hiyo katika runinga.

Pia Soma

“Kuwaona hao tumbili kutoka mataifa ya Afrika, bado hawafurahii kuvaa viatu.ilinukuu sehemu ya sauti hiyo ambayo ilimfanya Rais Nixon kucheka.

Hata hivyo, Naftali anadaiwa kwamba matamshi hayo ya kibaguzi yaliondolewa katika mawasiliano wakati kanda hiyo ilipotolewa mwakwa 2000 kwa sababu za faragha-wakati Rais Reagan akiwa hai.

“Mwaka jana kama mtafiti, niliomba mawasiliano yaliomuhusisha Rais Reagan yachunguzwe upya na wiki mbili zilizopita, mkanda mzima wa mawasiliano hayo ya mwaka 1971 yalitolewa.”

Alisema Reagan alikuwa amempigia simu Rais Nixon ili kumshinikiza kujiondoa UN.

Columnist: mwananchi.co.tz