Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Sababu za mzazi kumfundisha mtoto masomo yake nyumbani

10094 Saababu+pic TZW

Wed, 27 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Muda wa asubuhi ni kawaida kukutana na wanafunzi barabarani wakielekea shuleni huku sura zao zikionyesha hali ya unyonge kuashiria kuwa usingizi wao umekatishwa.

Hii inatokana na mazingira yalivyo, baadhi ya shule zipo mbali na makazi yao hivyo hulazimka kuamka mapema kuwahi vipind vya asubuhi.

Je mwanao yumo katika kundi la wanafunzi wanaoamka alfajiri kwenda shule?

Kama ndivyo ni wakati sasa wa kujaribu kuwa na darasa nyumbani kwa ajili ya kumfundisha mwanao kama mbadala wa kuepuka changamoto hizo.

Mtoto anaye amka saa 12 asubuhi wakati mwingine hulala darasani, hali hii humsababishia kukosa umakini wakati wa masomo hata ufaulu wake hushuka, mbaya zaidi ataichukia shule pamoja na walimu.

Zipo sababu mbalimbali za wanafunzi hao kuamka mapema moja wapo ni kuwahi kutokana na umbali wa maeneo wanayoishi.

Mwalimu mkuu Shule ya Msingi Mwandege, Azania Kimeru anasema mzazi kumfundisha mtoto wake nyumbani ni jambo zuri lakini atalazimika kumtafutia wenzake ili asiwe peke yake.

Kuhusu kudamka asubuhi anasema muda wa kuripoti shuleni ni kuanzia saa moja asubuhi, hivyo mwanafunzi anatakiwa kuingia rasmi darasani saa mbili kamili asubuhi kwa ajili ya kuanza vipindi.

Hivyo, changamoto hizo na nyingine zinaweza kupata suluhisho kama mzazi ataanzisha darasa kwa ajili ya kumfundisha mwanawe.

Fadhili Mohammed ni mwanafunzi wa darasa la nne shule ya Msingi Tandika, Temeke jijini Dar es Salaam yeye anaishi Toangoma anasema kila siku huamka afajiri kwa ajili ya maadalizi ya kwenda shule.

Mtaalamu wa saikolojia, Daniel Marandu anaeleza madhara ya watoto kukatisha usingizi hasa wakati wa asubuhi wanapoamka kwenda shule. Anasema kawaida mtu anatakiwa kupumzika kwa muda sahihi unaoshauriwa na wataalamu, hivyo kwa mwanafunzi hupoteza muda mwingi kutokana na changamoto za usafiri katika maeneo ya mjini. “Mwili wa binadamu ni kama gari, unahitaji kupumzika ukifanya kazi kwa muda mrefu unachoka na kusababisha madhara, ,” anasema.

Mtoto kuamka alfajiri kunauwezekano wa kumsababishia uchovu wa mara kwa mara unaoweza kumpunguza nguvu ya mwili. “Hapa utakuta mtoto anaanza kuwa msumbufu wakati wa kula na madhara ya tatizo hili hutokea akiwa mkubwa,” anasema.

Kuhusu kumfundisha mtoto, anasema ni jambo zuri ambalo litampunguzia adha mbalimbali, lakini anatakiwa kufundishwa na mtu aliyesomea taaluma ya ualimu.

“Jukumu la mzazi hapa ni kumsisitiza mtoto kufanya kazi hasa alizopewa na mwalimu. Siyo mbaya kumfundisha nyumbani, lakini wasiwasi wangu asije akaukosa ule msigi wa mwalimu, kwa sababu mwanafunzi anatakiwa afundishwe na mtu aliyesomea ualimu,”anasema mtaalaamu huyo. Zuhura Khamis ni mkazi wa Mbagala jijini Dar es Salaam anasema kumfundisha mtoto nyumbani ni jambo jema kwa sababu itamuandolea aza mbalimbali ikiwamo changamoto ya usafiri. Japo kwa mara ya kwanza mtoto atajiona mpweke kusoma peke yake nyumbani, lakini itafikia hatua atazoea. “Kwa jinsi mwanangu anavyoamka asubuhi kwenda shuleni, huwa namhurumia sana lakini sina jinsi kwa sababu anafanya hayo yote kwa faida yake ya baadaye,” anasema na kuongeza kuwa:

Kutokana na umbali wa shule (Mbagala hadi shule ya msingi Tabata), Wakati mwingine nilikuwa natamani apate likizo ili apumzike,”.

Alisema kumfumdisha mtoto nyumbani kwanza siyo tu mtoto atapata muda mzuri wa kupumzika bali kutapunguza gharama za usafiri. Zuhura anaeleza kuwa gharama nyingine kama sare ambazo zimekuwa changamoto kwa wazazi zitaepukika. Ametoa wito kwa wazazi watakaoamua kuwafumdisha watoto wao wawe wanauelewa, masomo mengine ni magumu yanahitajika mwalimu aliyesomea.

Anasema darasa hilo la nyumbani lisiwe kigezo kwa mtoto kutojichanganya na wenzake, hivyo wakati mwingine mzazi achukue watoto wengine awafundishe pamoja na mtoto wake. Zuhura anaungwa mkono na Hamis Omary mkazi wa Tabata relini, anasema kumfundisha mtoto nyumbani hasa anayeanza masomo ya awali ni kumpa muda wa kupumzika.

Anasema watoto wengi hasa wale wanaotumia usafiri wa shule wanaamka asubuhi sana na wakati mwingine hurudi usiku. “Mtoto kama huyu anatengenezewa mazingira ya kuchoka mapema hata atakapoanza elimu ya msingi, anaanza utoro kwa kusingizia kuumwa kwa sababu tu amechoka,” anasema Omary.

Mwalimu wa shule ya msingi Mabatini Temeke, Chiku Fortunatus anasema kabla mzazi hajaamua kuanza kumfundisha mwanawe nyumbani, kuna mambo muhimu anatakiwa kuyazingatia.

Moja ni kuangalia uelewa wa mtoto, mazingira mazuri ya kumfundishia na ufundishaji huo uwe endelevu. Mzazi pia anatakiwa kutoa nafasi kwa mwanaye angalau kila wiki akutane na wanafunzi wenzake kwa ajili ya kubadilishana mawazo. Pia, kama mzazi ataamua kumfundisha mtoto wake mwenyewe ni vyema akatenga muda angalau kwa masaa mawili kila siku na kutoa muda mwingi wa mazoezi muda wa masomo usipishane sana na ule wa shuleni ili asimjenjee mazoea ya uvivu.

Kumpa mazoezi ya Mara kwa mara ni muhimu kwa sababu yanapima uelewa wake kwa mile alichojifunza na kutopoteza muda wake kwa kulala au kuangalia michezo isiyokuwa na faida kwenye televisheni,”.

Anasema pia ni vyema mzazi akapata Mwalimu mwenye taaluma kwa ajili kufuatilia mwenendo wa mtoto wake. “Hii ni muhimu kwa ajili ya kuja maendeleo yake kielimu,”.

Haipotezi muda

Omari anasema anashauku ya kuwafundisha watoto wake wawili nyumbani kwani anadai muda mwingi unapotea bila sababu. “Kwanza akifika shule inabidi awasubiri wanafunzi wengine ambao wamechelewa waanze masomo kwa pamoja au wakati mwingine hawasomi kwa sababu Mwalimu hakihidhuria kutokana na sababu mbalimbali.”

Anaongeza kuwa wanafunzi wanakuwa wengi darasani hivyo hata ufuatiliaji wa Mwalimu kwa wanafunzi ni mdogo hivyo anasema unapomfundisha nyumbani ni rahisi kuelewa na anajifunza kwa haraka. “Nionavyo mimi kumfundisha mtoto nyumbani ni suluhisho mbadala wa kuepuka changamoto za usafiri hasa kwa wanafunzi wa mjini, kutembea umbali mrefu kwa wale wa vijijini pamoja na kuamka alfajiri cha msingi mzazi afundishwe kwa weledi au atafute mwalimu maalumu.”

Haina gharama.

Mwalimu Chiku anasema moja ya sababu kwa mzazi kuwa na uamuzi wa kumfundisha mwanawe nyumbano kwa sababu rahisi ukilinganisha na shule ambako analazimika kulipa ada.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirikisho la Watoaji Elimu Wasiotegemea Serikali Kusini mwa Jangwa la Sahara (CIEPSSA), Benjamini Nkonya anasema mwanafunzi anatakiwa kufundishwa na mtu mwenye taaluma. Mzazi kubeba hilo jukumu mwenyewe hawezi kufikisha ndiyo za mwanaye kielimu.

“Sikubaliani na jambo hilo la mzazi kumfundisha mwanawe nyumbani kama njia moja wapi ya kuepuka changamoto ikiwamo ya usafiri,” anasema.

Anasema mzazi anachotakiwa kukifanya siyo tu kuacha kumfundisha mwanaye nyumbani bali amuandikishe shule za karibu ili mtoto apate muda mzuri wa kupumzika.

Anasema kazi ya mwalimu ni kumpatia mwanafunzi maarifa kupitia taaluma yake. “Sasa huyu Mwalimu anataaluma ipi na je anauwezo wa kumfundisha ipasavyo kama inavyotakiwa afanye Mwalimu,” anahoji.

“Hizo changamoto za usafiri, kuamka alfajiri wazazi w anatakiwa kuboresha mazingira, kwa sababu wazazi wenyewe wanachangia katika hilo.”

“Na hili suala umbali kutoka mwanafunzi anapoishi hadi shule ilipo ni changamoto kubwa hasa katika maeneo ya vijijini, hivyo ni vyema wazazi wakakaa kama kamati ikiwezekana wajichange wapate kununua hata basi ndogo kwa ajili ya watoto wako,”

Columnist: mwananchi.co.tz