Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

SIASA ZA KITAA: Tunachoweza ni kumsifia Nyerere tu

76375 Nyerere+pic

Thu, 19 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Nyumba yake ya Msasani pale aliijenga kwa mkopo wa Benki ya Nyumba (THB). Ile ya Mwintongo alijengewa na jeshi miaka 10 baada ya kustaafu kutumikia Ikulu ya Magogoni. Huyo ndiye Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere. Hii leo kiongozi gani wa kuishi hivyo? Hakuna.

Waliobakia wanamuenzi kwa kumsifia tu. Lakini kuna mgomo wa kumuenzi kwa vitendo. Hata raia wenyewe ukistaafu ukiwa huna kitu kama alivyofanya yeye watakucheka hivi sasa. Watakuona bwege mtozeni uliyeshindwa kutumia vyema nafasi yako ya kutafuna mema ya nchi.

Yaani kiongozi wa umma kujilimbikizia mali ndio ujanja. Tumefikia hapo kama taifa. Raia nao wanaabudu mtu kujitwalia mali isivyo halali. Nani wa kuishi maisha yale aliyoishi Mwalimu? Hakuna. Wanachoweza ni kumpamba kwa mema aliyoyaacha ndani ya taifa hili na Afrika.

Miongo miwili sasa tangu tumpoteze mwamba huyu. Ambaye maneno na matendo yake, yalifanya tujiulize kama ni binadamu wa kawaida. Au alishushwa kutoka mbinguni na kupewa sura ya ubinadamu kama sisi? Kumsifia Nyerere ni rahisi sana. Kuishi kama Nyerere ni ngumu sana.

Mwezi ujao tutaendelea kuomboleza kama ilivyo ada. Ikiwa ni miaka 20 tangu atuache. Tuliobaki tujue kuwa kuahidi marehemu ahadi feki, ni kumtesa na kumuonea. Ni manyanyaso kwake kwa vile amekufa. Nani angependa akifa atendewe kama tumtendeayo Mwalimu?

Nani anamuenzi. Kama mtu anapata uteuzi leo kesho ana ghorofa? Nafasi zinatolewa kwa undugu, ukabila, ukanda na kidini? Nani anamuenzi kama wawekezaji wanakuja na kuondoa kwa gharama ya machozi yetu? Yakiyeyuka kwa jua au kupotea kama yale ya samaki? Nani ambaye anamuenzi Nyerere?

Pia Soma

Advertisement
Umesikia yanayoendelea Afrika Kusini. Ile ni chuki ambayo huishia katika uharibifu na vilio. Huzaa udhalimu unaodumu, kwani utawala unaojengwa kwa chuki hujiinua kwa udhalimu. Leo wanafanya alichopinga Mandela kwa makaburu (ubaguzi). Sisi huku tunaishia kumsifia Mwalimu tu.

kwamba tunamuenzi Nyerere. Lakini hatufanyi hivyo japo kila mwaka tunaadhimisha kumbukumbu ya kifo chake. Kitu ambacho tunakifanya kwa mazoea sasa kama tamasha la muziki. Hata mwaka huu watu wataishia kujadili mazuri yake na kisha kuyaacha kama yalivyo.

Columnist: mwananchi.co.tz