Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

SIASA ZA KITAA: Siasa na wasomi dili ndani ya dili

56265 Dk+levy

Wed, 8 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dili kubwa Afrika na Tanzania ikiwemo kwa sasa ni siasa. Wahadhiri na wasomi wanatoweka vyuoni kama sauti za tausi pale Ikulu. Wanajiingiza kwenye siasa na harakati za kipuuzi kwa mgongo wa demokrasia. Wamechoka kuchakaa kwa vumbi la chaki.

Badala ya kufundisha watoto vyuo vikuu. Wameacha kusaidia kama taifa tujikwamue. Wanatumia uwezo wa akili zao kuwaandikia wazungu ‘propozo’ za kuomba mkwanja. Wakipewa wanaenda kwa watu masikini na mapoyoyo kuwauliza nani maarufu kati ya mpinzani na mwenye madaraka.

Umaarufu wao unamsaidia nini mama yangu kijijini? Asiyejua utamu wa maji safi tangu taifa hili liundwe na kina Nyerere na wenzake?

Wanapewa mabilioni ya pesa wanayatumia kwa maswali ya kipuuzi kwa mtu ambaye hajui hata zahanati inafanaje?

Na sisi watoto wa mjini tunachekelea tukiambiwa na hawa wasomi kuwa huyu maarufu kuliko yule. So what? Wasomi hawatumii usomi kutusaidia. Bali wanataka kuingiza pesa kwa ‘propozo’ za ajabu. Ukiuliza, eti demokrasia. Hawa wapelekwe jela kwa utakatishaji wa pesa.

Wengine ruzuku inawaondoa kwenye ramani ya siasa taratibu. Wanawaza pesa. Wanasiasa wanapiga kelele majukwaani ili wapate ajira kwa mgongo wa kutetea maslahi ya Taifa. Na wahuni wanaojificha kwenye kivuli cha usomi wanaendesha harakati za kihuni ili wapate pesa za wazungu.

Mtu anaanzisha kitaasisi cha kutetea haki za binadamu. Lakini shughuli za hicho kitaasisi hazina tofauti na za vyama vya siasa. Ukweli ni kwamba wanasiasa na wasomi wa Afrika, wanatumia matatizo ya watu kujineemesha tu. Hawana chembe ya uzalendo wala uchungu.

Kama mkubwa anachemka kwenye usukani wake, mwacheni apotee maboya ili 2020 akose kura. Na iwe ‘veri simpo’ wengine kuikalia magogoni kwa makosa yake. Na kama yuko vizuri, kwanini asiwakaushie washindani

wapige makelele yao kwa mikutano na maandamano? Kama anafanya vyema, makelele yao hayana madhara. Wananchi wakiambiwa mabaya yake wakati anafanya vizuri nani atawaelewa? Mikutano inamzuia nini Jenista kufanya kazi yake? Kuna vitu vingi sivielewi lakini hili la kupiga stop makelele ya wapinzani hakuna anayeelewa.

Demokrasia imeletwa kama dini zilivyoletwa kutoka magharibi au mashariki. Tunaambiwa dini imekuwa biashara. Hata demokrasia ni biashara pia. Tukitaka kusonga tuwapuuze wanasiasa na wanaharakati wachumia tumbo. Huhitaji msaada wa FBI kuwajua wachumia tumbo. Maana wako wazi kama vazi la kahaba.



Columnist: mwananchi.co.tz