Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

SIASA ZA KITAA: Makonda achana na Pierre, vijana werevu hawapo

50214 Dk+levy

Thu, 4 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kuna jamaa alikuwa anamiliki kiwanda cha nguo za ndani. Alipata wakati mgumu baada ya kugundua kila siku kuna upungufu wa nguo hizo kiwandani kwake. Wakaguzi wa hesabu hawakuwahi kuona tofauti. Ikabidi aweke upekuzi wakati wa kutoka kwa kila mfanyakazi kukaguliwa.

Licha ya zoezi hilo kuendeshwa kila siku, hakuna mfanyakazi aliyewahi kukamatwa. Na bado mzigo kwenye ‘stoku’ uliendelea kupungua kila siku. Wafanyakazi wote walikuwa wakitoka na kukaguliwa wanakutwa na nguo moja tu ya ndani. Kwa sababu mmiliki huyo alidhani pengine wafanyakazi hao wakitoka wanaiba na kuzivaa mbilimbili au zaidi.

Siku moja akiwa amejikatia tamaa, kuna dada ambaye ni mpishi wa chakula alimfuata bosi huyo na kumuomba nafasi ya kuongea naye. Alipokubaliwa akamwambia bosi huyo kuwa muda mrefu anamuona akihangaishwa na upungufu wa nguo za ndani pale kiwandani.

Akamshauri kuwa badala ya kukagua wafanyakazi wanapotoka kwenda majumbani, aamuru walinzi wakague kila mfanyakazi anapoingia kiwandani. Japo hakuelewa moja kwa moja ushauri wa yule dada kutokana na nafasi yake na elimu ndogo, lakini akaagiza kisiri walinzi wafanye hivyo kesho yake.

Alishikwa na mshangao. Baada ya kuambiwa kuanzia wakurugenzi mpaka wafanyakazi wa chini hakuna aliyekutwa na nguo ya ndani. Dada mtoa ushauri hivi sasa kapanda cheo, ni mmoja wa wakurugenzi wa bodi kiwandani pale. Huyo dada siyo wa kizazi hiki. Dunia ya sasa hawazaliwi werevu.

Makonda wiki iliyopita alimponda Pierre Liquid kama mtu wa ovyo anayepewa kipaumbele. Huku werevu kama Jokate wakikosa sapoti. Anayesema hana sapoti ni kijana aliyepewa ukuu wa wilaya (sijui sapoti ipi anataka). Na ndiye aliyemwalika Pierre na kuchangia laki moja. Watu wakashangilia kauli ya Makonda.

Mwisho waliomshangilia wakamgeuka kesho yake. Ni kwa sababu hawana werevu wa kugundua kosa mpaka waambiwe ni kosa. Makonda alimdhalilisha binadamu mwenzake kwenye tukio lililoandaliwa na kiongozi mwenzake. Ina maana mtu wa ovyo alialikwa na kiongozi mwenzake.

Ina maana Pierre ana utofauti sana na lile kundi lililokusanywa kwenda kuhamasisha pambano la Taifa Stars na Uganda? Kama wale ni werevu sana kuliko Pierre basi neno werevu linahitaji kudadavuliwa upya maana yake.



Columnist: mwananchi.co.tz