Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

SIASA ZA KITAA: Hakuna mtu wa ovyo, tunapenda vitu vya ovyo

54957 Dk+levy

Wed, 1 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, “hatuwezi kuwa na kiongozi ambaye hatujui kesho ataamka na nini au kashauriwa nini na mkewe”. Leo kauli yake inaleta maana halisi, kwani wengi wetu hatujui kesho itakuwaje. Nani atafukuzwa, atatenguliwa au kuteuliwa? Na kibaya zaidi tumeamua kuishi kwa matumaini ya ahadi kuliko hali halisi.

Mwanzoni likitokea lolote fasta Mwamba angetoa kauli ‘onze spoti’. Kwa sasa yupo kimya. Hilo pia hufanya raia tusijue kesho tutaamkaje. Siasa yetu ilipofika sioni haja ya Mwamba kuwa msiri au kutushtukiza. Anaweza kuwa na mikutano na wazee kila mwezi kama watangulizi wake. Kuelezea mambo muhimu ama ateua mtu wa kutupatia ripoti.

Hatujui bei ya sukari itapungua kwa kurekebisha viwanda, kuongeza uzalishaji, kuruhusu sukari ya nje, kuvamia ‘godauni’ za watu. Au kupiga marufuku unywaji wa chai. Ukimtazama usoni na kauli za Mwamba wa Magogoni, utakiri ana nia ya dhati kututoa hapa. Swali je, ana watu wanaojua ni wapi anakotaka kutupeleka kama taifa?

Ukiangalia Bunge ili uone kama mawaziri wanaweza kuonesha uelekeo, utachanganyikiwa zaidi. Wako ‘bize’ na miongozo, kuhusu utaratibu, taarifa na kujibu vijembe vya kina Mnyika na wenzake kuliko kueleza hali halisi.

Kuna mzee aliniambia unaweza kuwa dereva mzuri unayefuata sheria vyema, lakini hujui unaenda wapi. Kutokujua unakokwenda kwa lugha ya ‘mabeberu’ ni kupiga ‘makitaimu’. Upo upo tu.

Taifa haliendeshwi kwa kauli za Rais tu. Ndiyo maana ya uwepo wa Katiba, ilani, sera, sheria na nyaraka mbalimbali. Na kuhoji, kukosoa, kushauri, kulalamika kama mambo hayaendi, ni haki yetu. Tatizo Bongo kuhoji ni kukosa uzalendo. Wabunge wanaotakiwa kuhoji, kukosoa na kushauri ndio wanaongoza kampeni ya kutohojihoji vitu. Tabia hii haiwezi kutupeleka popote.

Kisiasa kuna kiporo cha Katiba Mpya. Lakini ukifuatilia hotuba za mawaziri bungeni, utaelewa kwa nini Pierre ni maarufu kwa maneno yasiyozidi matano tu. Unakumbuka kauli ya Paul Makonda juu ya kuendekeza watu wa ‘ovyo’ na kuwapa umaarufu wa bure? Nchi nzima ilimgeuka mpaka viongozi. Akabaki peke yake akipambana na hali yake. Namna raia walivyowaka mitandaoni na mitaani, serikali yote na Bunge likawa nyuma ya Pierre. Ile ndio maana ya nguvu ya umma inapoamua kusimamia kitu.



Columnist: mwananchi.co.tz