Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

SIASA ZA KITAA: Dhambi ya mtandao inaweza kuitafuna hata Chadema

90181 Mitandaopic SIASA ZA KITAA: Dhambi ya mtandao inaweza kuitafuna hata Chadema

Mon, 30 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tangu 1995, Jakaya Kikwete ni kama alituroga Wabongo wote. Tuliamini kwamba baada ya Mkapa kuondoka pale Magogoni anayestahili kutuongoza ni yeye. Katika hili huenda mimi nilirogwa zaidi ya wengine. Sikusikia la muadhini wala mnadi swala juu yake mwaka 2005.

Jamaa alijipanga. Aliusuka mtandao wake. Alitengeneza njia na mwelekeo wa nchi atakavyo. Jamaa alifanya anavyotaka juu ya fikra zetu kisiasa. Hata viongozi wa vyama pinzani walitaka Jakaya awe Rais.

Ushindi wake wa 2005. Ulikuwa muunganiko wa mvuto wake, mipango ya CCM na fitina za mtandao wake.

Mtandao wake ukiteketeza wapinzani wake ndani ya CCM. Mipango ya CCM ni pamoja na pesa za EPA kutumika. Huku mtaani wengi walitekwa na mvuto wa Jakaya mwenyewe. Alikuwa noma sana jamaa.

Lowassa alijaribu kupita njia zilezile za Jakaya 2015. Tena akiwa kajipanga zaidi. Tatizo alipambana kimtandao na mtandao waliousuka wao wenyewe. Akaishia kwenye korido za Ufipa Kinondoni pale, akipishana na kina Dk Slaa. Mchezo na ndoto zake za urais zikaishia hapo. Sikushangaa kurudi kwake CCM.

Ulitaka aende wapi? Akafanye nini katika majukwaa ya siasa 2020? Mwakani atakuwa na miaka 67 kama sijakosea. Muda mzuri wa kupumzika na kualikana kwenye tafrija za wastaafu wa chama na serikali.

Mwaka 2015 kila mtu alikuwa na ndoto za kupanga miaka 10 pale Magogoni. Wingi wa wagombea lengo ilikuwa ni kumdhibiti Lowassa na kambi yake.

Pia waliojitokeza wengi waliamini inawezekana kuwa rais kirahisi kama JK wa 2005. Wakiamini urais ni kumiliki mtandao. Mitandao ya chama ikawa mingi kuliko ya simu.

Umefuatilia chaguzi ndani ya Chadema? Kuna ‘Ujakaya’ mwingi sana. Hawaamini katika uwezo wa mtu tena. Wanaamini katika mitandao na kambi ndani ya chama kama wakimbizi wa Kasulu.

Hii ni dhambi ya mtandao wa tangu 1995. Siasa za Tanzania zinaendeshwa kwa msingi ya mitandao. Hii ni dhambi ya kidemokrasia.

Unaenda muongo wa tatu sasa. Siasa zinaendeshwa kwa akili ya mtandao. Mwenye mtandao na fedha nyingi, anaweza kuwa yeyote ndani ya chama chochote. CCM wanaishi katika kofia ya hofu kwa mwenyekiti taifa.

Chadema wanaishi katika hofu na imani ya mtandao na kambi ndani ya chama. Jipe muda kisha fuatilia.

Columnist: mwananchi.co.tz