Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

SIASA ZA KITAA: Dhambi kubwa mtu kulazimisha apendwe

60285 Dk+levy

Thu, 30 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mtu yeyote au kiongozi awe wa kijamii, kidini au wa kisiasa unapolazimisha upendwe ni dhambi kubwa. Kama mtu hakupendi mpe na nauli kabisa aondoke zake. Ama sivyo unaiua thamani yako wewe binafsi, taaisisi yako, chama chako na yule aliyekuumba. Na hata raha ya uongozi wako hakuna. Ukipendwa kwa hiyari utaheshimiwa.

Usipoteze thamani ya muda na thamani yako kwa kujaribu kuhonga hata kwa kukenua meno ili upendwe na watu. Upendo huja wenyewe bila kulazimisha. Asiye na upendo kwako, achana naye au mpe nafasi akapende mahala pengine. Fanya kitu ambacho kitamfanya akuelewe na si kumlazimisha.

Mwili ni kama taifa lenye kila aina ya madini ya thamani. Ukijichukulia poa unakaribisha wawekezaji wa hovyo. Ambao watakuchukulia kirahisi kwa kukuchimba wakuache kama handaki lenye popo. Mume au hata mke au kiongozi wa kisiasa huhitaji nguvu kubwa ili upendwe. Timiza wajibu na ahadi zako upendwe mpaka ukereke.

Uwe mbunge, diwani au kiongozi mwinginem askofu mchungaji n.k, huwezi kupendwa na kila mtu, labda kama wewe ni pesa.

Unaweza kuwapenda wakwe, mashemeji, mawifi na ukoo wote wa mume au mke wako, lakini usipendwe na mke au mume mwenyewe, licha ya kujitoa kwake na kwao.

Ni maisha jinsi yalivyo. Kisiasa pia unaweza kuwa kiongozi mzuri, lakini watu hawakutaki. Hapo usilazimishe buluu kuwa kijivu, utaishia kufanya mambo ya ajabu dhidi ya watu.

Pia Soma

Chukuliwa mfano wa madikteta duniani tangu enzi na enzi, tatizo lao kubwa ni kutaka kila mtu awapende. Angalia kina Adolf Hitler, Benito Mussolin ndivyo walivyokuwa. Mtu anataka atazamwe vizuri, aongelewe kwa mema, ajadiliwe kwa kusifiwa na kila mtu.

Hapo lazima hapo ‘utadata’ au inakuwa ‘shotikati’ ya kuukaribisha wendawazimu walioupata kina Bokassa nyakati zile.

Ukitaka raia akutukuze tenda kile anachotaka umtendee au ulichoahidi kumtendea. Nje ya hapo utajikuta unatumia njia za wazi na giza kuficha ukweli. Na dawa ya raia ni ukweli, na ukweli uwe kwa pande zote mbili. Timiza ahadi yako kwao na wao watimize kwa kuungana nawe kwenye kila ufanyalo. Mwisho huwa ni furaha tu.

Columnist: mwananchi.co.tz