Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

RIPOTI: Finland yaongoza nchi zenye furaha duniani, Burundi, Tanzania, Rwanda zashika mkia

4833 Kariakoo 02 TZW

Sat, 17 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Ripoti ya mwaka 2018 ya nchi zenye furaha zaidi duniani iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa chini ya taasisi ya ‘Sustainable Development Solutions Network and the Earth Institute’ imeonesha kuwa Finland ndiyo nchi yenye watu wenye furaha zaidi Duniani ikifuatiwa na Norway ambayo mwaka 2017 iliongoza kwenye orodha hiyo.



 

Ripoti hiyo ambayo imehusisha nchi 156 duniani imeonesha nchi nyingi za Afrika zimeshika nafasi 10 za chini kwenye orodha hiyo ambapo Burundi, Afrika ya Kati, Sudani Kusini, Tanzania, na Rwanda z.

Nchi nyingine zilizoingia kwenye 20 bora ya nchi zenye furaha zaidi ni Denmark, Iceland, Switzerland, Uholanzi na Canada.



Marekani na China licha ya kuwa nchi zenye uchumi imara lakini wananchi wake wameonekana kutokuwa na furaha, ripoti hiyo imesema kuwa ni kutokana na mgawanyiko wa masuala ya kisiasa.

Marekani mwaka 2017 ilikuwa nafasi ya 14 mwaka huu imeshika ya 18, huku India na China zikishuka nafasi 7 ukilinganisha na mwaka jana.

Kwa upande wa nchi 10 za mwisho au zilizoshika mkia kwenye orodha hiyo ya nchi 156 zenye furaha zaidi imo Burundi ambayo ni ya 156, Afrika ya Kati 155, Sudan Kusini 154, Tanzania 153 imesalia kwenye nafasi yake ya mwaka jana na Rwanda ya 151.

  • Burundi
  • Central African Republic
  • South Sudan
  • Tanzania
  • Yemen
  • Rwanda
  • Syria
  • Liberia
  • Haiti
  • Malawi
Nchi ilizofanya maajabu kwenye ripoti hiyo kutoka Afrika ni Togo ambayo imepanda kwa nafasi 18 kutoka nafasi ya mwisho mwaka 2015, nakuifanya itoke kwenye orodha ya nchi zilizoshika mkia.

Sababu za nchi nyingi za Afrika ikiwemo Tanzania wananchi wake kukosa furaha ni Magonjwa, Viribatumbo, Madeni, migawanyiko/mipasuko ya kisisasa na msongo wa mawazo.

Soma zaidi ripoti hiyo -> World Happiness Report 2018
Columnist: bongo5.com