Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Nini kimejificha kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa?

83269 Uchaguzi+pic Nini kimejificha kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa?

Sun, 10 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwaka 2014 na ule wa mwaka 2009 wananchi walikuwa na hamasa kubwa ya kushiriki.

Uchaguzi huo wa ngazi ya kwanza ya uongozi wa Serikali unahusu wenyeviti wa kijiji, wenyeviti wa mitaa, wajumbe wa halmashauri ya kijijiji na wajumbe wa kamati za mitaa.

Katika uchaguzi wa mwaka 2014 vyama vya upinzani viling’aa zaidi ukilinganisha na wa mwaka 2009.

Hata aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Kharist Luanda, alinukuliwa akisema ushiriki wa vyama vya siasa ulikuwa mkubwa kutokana na vyama 15 kushiriki.

Pamoja na kwamba vyama vya upinzani vilipata viti vingi katika uchaguzi wa mwaka 2014, Chama cha Mapinduzi (CCM) kiliendelea kuongoza kwa kuibuka na viti vingi zaidi.

Katika nafasi ya wenyeviti wa vijiji CCM kilipata viti 9,378 (asilimia 79.81), vitongoji 48,447 (asilimia 79.83) na kwa mitaa 2,583 (asilimia 66.66.).Kwa upande wa wajumbe serikali za vijiji na mitaa, CCM kilipata 100,436 (asilimia 80.24) na wajumbe wa viti maalum 66,147 (asilimia 82.13).

Wakati huo vyama vya upinzani viliungana kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na kuleta hamasa kubwa ya wananchi kushiriki katika uchaguzi.

Hata aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye baada ya kutangazwa matokeo ya kwanza kabla ya marudio, alikiri ushindi wa chama hicho ulipungua kwa asilimia 12 kutoka asilimia 96 za mwaka 2009 hadi asilimia 84 mwaka 2014.

Hamasa ya wananchi kushiriki katika uchaguzi pia ilionekana katika uchaguzi mkuu 2015 kiasi cha wanasiasa kueleza kuwa hali hiyo haijapata kutokea tangu nchi itape uhuru.

Kwa undani wa habari hii pata nakala ya Gazeti la Mwananchi.

Columnist: mwananchi.co.tz