Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Nani adui wa rais wetu? nani adui wa taifa letu?

89011 Aduipic Nani adui wa rais wetu? nani adui wa taifa letu?

Wed, 18 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tanzania ni yetu sote, ni lazima tushirikiane kuijenga, kuilinda na kuirithisha salama kwa vizazi vijavyo. Wale wote wanaotoa maoni yao, si kwamba wanampinga Rais wetu na si kwamba hawampendi. Kumekuwepo na upotoshaji kwamba watu wanampinga Rais wetu na hawampendi. Mawazo haya si mazuri maana yanalenga kumchonganisha Mheshimiwa Rais na wananchi wake. Pia yana lengo la kuuficha ukweli ili wale wanaonufaika na hali ya Mheshimiwa Rais kutoambiwa ukweli, waendelee kuneemeka wao na familia zao. Kinachofanywa na wale wanajitokeza kutoa mawazo yao juu ya hali ya Taifa letu, ni kuchangia, kuboresha, kuongezea kwa nia moja ya kuleta maendeleo ya haraka katika taifa

Lengo la makala hii ni kusisitiza hoja yangu ya kumuunga mkono Rais wetu, na kukumbusha kwamba kinachohitajika sana katika Tanzania ya leo ni matendo zaidi ya maneno matupu. Tuache “unafiki”, ili tuweze kulijenga taifa letu.

Hitaji lililo mbele yetu sasa hivi ni kufanya kazi kama wendawazimu, ni uwajibikaji, uaminifu, uzalendo, kulinda maslahi ya taifa na kujenga mshikamano katika taifa letu. Haya hayawezi kuja kwa maneno matupu! Panahitajika mifumo imara ya kuliendeleza taifa letu. Hivyo ni lazima tukae chini na kutafakari, tujadiliane hadi kufikia makubaliano. Ni lazima watu wajadili vijiweni, kwenye daladala, kwenye mikutano, kwenye starehe, kazini na kwenye semina. Ni lazima watu watoe mawazo yao kwa kuandika makala, vitabu nk. Hata kama inalazimika ni bora kuwa na mjadala wa kitaifa kuhusu uhai wa taifa letu la Tanzania.

Taifa letu bado lina changamoto nyingi. Katika makala hii nitatoa tatu ambazo mimi ninaona ni muhimu na zinahitaji kufanyiwa kazi ya haraka.

Kwanza, changamoto ya kazi ambayo haijakamilika. Haikukamilika katika uongozi wa awamu ya kwanza, ya pili na hata ya tatu, ya nne na sasa hii awamu ya tano nayo ni kazi kuondoa umaskini na ubaguzi katika jamii yetu. Watanzania wengi bado ni maskini. Maisha yanakuwa magumu kupindukia. Sote tunafahamu mshahara wa kima cha chini cha Mtanzania. Kutojadili hali hii waziwazi, kutomweleza Rais wetu waziwazi hali hii, na badala yake kushangilia na kumsifia kwa mafanikio, ni dhambi kubwa. Wanaomficha hali hii, ndiyo adui wake.

Vijijini pia kuna umaskini mwingi na maisha yako juu. Lakini watu wa vijijini wana maisha ya kutokuwa na huduma kama maji safi na salama, matibabu yenye kiwango, nyumba nzuri, chakula cha kutosha na mengine mengi ambayo yanaweza kuwaletea maisha bora. Hali hii ni lazima ijadiliwe waziwazi bila unafiki. Kuficha hali hii na kuendelea kushangilia kwa nyimbo na maneno ya kupamba ni dhambi kubwa. Kuficha ugonjwa, ni kosa lisilokuwa na msamaha!

Ubaguzi wa kabila, dini, rangi na jinsia ni kazi ambayo hatujaikamilisha. Haikukamilishwa wakati wa uongozi wa awamu zoter. Pamoja jitihada zinazofanyika za kuwateua wakuu wa wilaya, wa mikoa na majaji wanawake, bado ngazi za Juu katika uongozi wa taifa letu zinashikiliwa na wanaume. Hii inaonyesha kwamba bado tuna njia ndefu ya kwenda katika swala zima la usawa wa kijinsia.

Columnist: mwananchi.co.tz