Dodoma. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communication Limited (MCL), Francis Nanai amewataka wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) kujipanga kwa maisha wanayoyataka baadaye.
Nanai ameyasema hayo leo Jumamosi Juni 8, 2019 katika ukumbi wa Chimwaga wakati akizungumza katika warsha ya kujadili maendeleo ya kitaaluma chuoni hapo iliyowashirikisha pia wahitimu wa miaka nyuma walio katika ajira na waliojiari.
Katika warsha hiyo iliyokuwa na kauli mbiu ya maendeleo ya kitaaluma mara baada ya kumaliza masomo ya sayansi Udom Nanai amesema, "Lazima upange katika maisha yako unataka kuwa nani? Na baada ya miaka mingapi unataka uwe umefika hapo. Na utengeneze njia ya kufikia hapo."
Amezitaja njia za kutengeneza katika kujipanga maisha unayotaka ni pamoja na elimu, uwezo wa kujieleza na kuwa na tabia nzuri.
“Tunapoajiri tukishaangalia vyeti, tunaangalia nini hasa kinakutofautisha na wengine. Tunaangalia tabia ukiwa na tabia mbovu huwezi kupata ajira ,”amesema Nanai aliyekuwa akiwasilisha mada ya maendeleo ya taaluuma na ujasiriamali.
Rais wa wanafunzi katika chuo hicho, John Bosco amesema ni vyema mafunzo hayo yakatolewa wakati wanapoanza mwaka wa kwanza ili kujiandaa mapema.
Pia Soma
- VIDEO: Hivi ndivyo mfanyabiashara aliyetajwa na Magufuli alivyowazungusha TRA, kugoma kuwapa rushwa
- Makonda: Nikiwepo 2020 wabunge Dar wasiotatua kero za wananchi wahesabu maumivu
- Halima Mdee afanyiwa upasuaji Dar, atoa neno