Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

NDANI YA BOKSI: Pedeshee Uwoya, tuma na ya kutolea basi...

67720 Pic+uwoya

Mon, 22 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Khadija. Mmoja kati ya warembo bora kuwahi kukutana naye kwenye maisha yangu. Ana umbile sahihi ambalo naamini mpaka malaika wanapata wivu wakimuona. Ngozi tamu na macho ya kuvutia. Achana na lips zake zilizovimbiana kama zimeng’atwa na nyigu

Mara ya kwanza kukutana naye ni miaka mingi nyuma. Nyerere na Mtikila wakiwa hai. Lakini mpaka leo anabaki kuwa alama ya mrembo wa asili. Alipendwa mpaka na mchanga alioukanyaga. Nyasi zikimtetemekea. Na madereva wakivimba vidole kwa honi wamuonapo barabarani.

Sikuhisi vibaya akisemeshwa au kukonyezwa njiani. Bali nilishangaa asipofanyiwa hayo na wakware. Mtu pekee ambaye asingeweza kufanya hayo ni mlemavu wa macho tu. Mpaka mademu wenzake walimtamani. Mwaka wa saba huu Khadija yupo Segerea. Kwa kesi gani? Tuyaache hayo.

Wasichana wazuri aina ile hawazaliwi siku hizi. Hawa wa leo huzaliwa kawaida kisha hukuzwa na mapambo. Zamani msichana akivunja ungo umbile lake hutanuka. Ngozi huwa nyororo na kifuani huota vitu ‘flan amazing’. Hivi sasa msichana anavunja ungo akiwa kaunta bar.

Nywele zimepandikizwa katani nyeusi wanazoita wigi. Kwenye macho utadhani kaweka makuti ya minazi ya Ikwiriri. Eti kope bandia. Ngozi ya uso huwabadilika kama miale ya mvua za vuli. Shavu la buluu na komwe la pinki, huku midomo ikiwa ya udhurungi. Kituko.

Siku hizi kila kitu ni kibaya. Sukari si nzuri, chumvi si nzuri, nyama nyekundu si nzuri, soda si nzuri. Chakula cha kuunga si kizuri, pia kutumia gari sana kiafya si vizuri. Kama vile haitoshi, eti pombe si nzuri, sigara siyo nzuri, miale ya mwanga wa simu au computer si mizuri.

Pia Soma

Wanaotuambia hivi vitu si vizuri, ni wale waliotuletea kwa matumizi, na vitu walivyokuta tunavitumia walividharau. Ni kama kutuletea hizi tawala za kisiasa kwa kutuaminisha kuwa tawala za Kichifu hazikufaa. Leo tuna rais wa tano tangu tupate uhuru. Lakini yule aliyetutawala bado yuko chini ya Malkia Elizabeth.

Tuachane na hayo. Kwa wale ambao mambo ya kiafya hayako mzuka. ‘They need not to worry out coz those are God’s will’. Au sio? ‘Any way’, wazee mnaonaje ukali wa maisha? Maana since 2015 vitu vina ‘rise’ bei kwa kasi ya ajabu halafu cha kushangaza ‘salary’ dizaini kama ime-freeze tu. Ime-freeze ndiyo!

Maana kuniongezea buku mbili katika amount yangu ya kawaida naona unazingua tu. Unaniongezea ‘two thousands’ halafu kila kitu kimegoo high maana yake nini? Kama si kunisanifu tu. Waheshimiwa, ‘please we are begging you’, tuangalieni basi nasi hata kwa jicho la huruma.

Jicho lenye kuitambua angalau thamani yetu in this state. Dhiki inatufanya tunachakaa. Kama tungekuwa vyuma siku nyingi tungekuwa pande za Kariakoo Gerezani tunapimwa. Life hii inatufanya tuonekane ‘Scrapers’. Ukata unatupotezea thamani ya utu. ‘Day by day’ hali inazidi kuwa tight.

Mabosi ‘you need to know that, the peace you talk about on stages can’t remain’ katika hali kama hii. Hali ya kila siku bora ya jana. Kwani mnafikiri nasi hatujui utamu wa maisha mazuri? Au mnadhani hatuoni tofauti yenu na sisi? Kama ‘situation’ imewashinda ‘you need to break the news’ tujue.

Mnatufanya tuone mkosi ‘to be born in this Land’. Wakati sisi wimbo wa shida ukiwa umetuchosha. Nyie hata hamuonekani kutukumbuka huku juani mlipo tutupa. ‘If you have never dumped us, why don’t you need to change the situation, so that we can get some relief of this disturbing life?’

Katika mshahara wa laki unusu, mchele wa buku tatu, nauli mia sita hamsini kweli tutafika? Hali hii ni tete hasa. ‘Life is so harder on our side!’

Maisha yanafanya watoto badala ya kwenda shule wanafikiria pesa ya kula. Wanaobeti ni wengi kuliko walio madarasani. Msoto zaidi ya jela!

Kumbuka tu kuwa ‘70 percent ya population ya this country ni vijana’. Do you know how most of them run this life? Ni vichekesho. Hali mbaya! Life yao ni kama wanaigiza mchezo wa kachupi. Sura zao zimekata tamaa ni kama mfungwa asiye na hatia. Yule anayesubiri dakika tu atiwe kitanzi.

Wengi kati yao wanaamka bila kujua kitu watakachokula. Maisha yao si tofauti na wakimbizi. Tupia jicho lako ‘on the street you gonna see them’. Wanaranda majalalani kutafuta machupa kwa saa zaidi ya nane. Kisha hela yao kuisha kwa dakika kumi. ‘Inflation’ ilivyo nuksi!

Sasa katika hali hii tutegemee nini? Kama nguvu kazi ya taifa hili iko in dire poverty, nini tutarajie? Hawajishughulishi? Hapana! Ni vile tu hali ya uchumi inavyobana. Akipata buku tano katika hustling hizi atafanyia nini? Ni ubwabwa kwa Mama Lishe, itakayobaki afanye nauli ya kurudi kwao.

Huwa najiuliza hivi hawa wavaa suti na tai hali hii hawaioni? Au wanatuchukulia sisi ni madaraja ya neema zao? Manafasi ya dwasi waliyonayo kwetu yana faida gani? Hatuwezi kusomesha watoto Ulaya kama nyinyi. Lakini basi fanyeni mpango kamba ya ‘life’ ilegee kidogo.

Maana mambo si mambo tena. Hapa town katika sura ya nchi hali iko hivi? Je huko Matombo mabondeni na Ugweno Milimani? Kuna kitu tunakiona baina yenu na sisi. Tuna tofauti kubwa sana ya kimaisha. Life hii ni ‘too tough’, raia wanasagika kama si kupigika.

Ma-honourables, mnatakiwa mfanye hima mambo yakae sawa. Hatuutaki ule msemo wa kama mbwai na iwe mbwai vichwani mwetu. Mabishoo na maduu kitaa wanataka unafuu wa maisha. Propaganda za amani na historia ndefu kama Isidingo The Need, kwa sasa zinachosha. Tunataka kitu kipya zaidi.

Karne ya ishirini na moja hakuna Mtanzania mjinga. Hali ikiwa hivi hivi, itafika wakati wa Masaki na Tandale wote tutakua njia moja. Hebu tutazame hili kidogo. Tulizoea wanamuziki wa dansi kutuzwa mkwanja na mapedeshee. Kisha waandishi kuandika Twanga Pepeta wamwagiwa manoti jukwaani.

Leo hii hali ni tofauti sana. Irene Uwoya msanii wa filamu. Anawatuza kwa kuwarushia noti wanahabari kama wanamuziki wa dansi. Wakati wakizidaka hizo noti na kushangilia, wasanii wenzake hasa ukimuangalia vizuri yule mmoja, wanatazama kwa shauku na matamanio. Katazame ‘clip’ uone sura ya mmoja aliye pembeni na wenzake wengine.

Tunarudi pale pale. Kwamba warembo kama kina Khadija hawazaliwi tena siku hizi. Hata wanahabari wa sasa ni tofauti ni wale wa kipindi cha kina Khadija. Alichofanya Uwoya ingekuwa zamani angejizika kisanii palepale. Lakini wanahabari wa online TV (kizazi kipya) kwao ni ujiko.

Siku hizi kila mtu mwenye simu janja (smart phone) ni mwanahabari. Wakati zamani watu wakifeli masomo ya sayansi na mengineyo walikimbilia polisi. Hivi sasa madogo wakifeli Udiamond, na Uwema Sepetu kama siyo Usteve Nyerere. Wanaamua kuwa wanahabari (online TV).

Ndo hao wanaodaka elfu kumi kumi za Uwoya na kuchekelea kama mazuzu. Mara kadhaa husikia Spika akilalamika kuwa Mhimili wa Bunge umedharauliwa. Sasa ni zamu ya wanahabari. Yote hii ni kwa sababu ya ukata. Maisha ya kuungaunga kama maneno ya mwenye kigugumizi.

Ukitazama sura ya fulani na wasanii wenzake. Unagundua nao walitamani kutupiwa zile noti. Aliishi hivi Jack Wolper kipindi fulani na kugeuka pedeshee mjini. Akafuata Wema Sepetu na mbwembwe zake. Hata Kajala alishafanya fujo za namna hii kabla ya Irene Uwoya.

Soko la filamu haliwezi kusimama kwa uduwanzi huu. Uduwanzi ambao ni sehemu ya chanzo cha kifo cha soko lenyewe. Wakati Wema na Wolper wakifanya fujo hizi, takataka nyingi ziliingia kwenye tasnia kwa kuwaza utajiri. Zikiamini wametajirika kwa sanaa. Kumbe ni kipato cha nje ya sanaa yenyewe.

Hivi sasa Irene ndo totoz ya Bongo Movie inayokimbiza. Macho na mavazi yanaashiria pesa. Tabasamu lake linakupa picha ya kiumbe uzao wa Eva, kinogeshwacho na uwepo wa noti nyingi kando yake. Je, ni noti za soko la filamu zake? Let me sign out, coz kuna ‘chick’ anataka tukameet. Kama vipi next time.

Columnist: mwananchi.co.tz