Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Mwandishi wa Mwananchi kuzikwa Muleba

50862 Pic+mwandishii

Sun, 7 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Mwili wa aliyekuwa mwandishi wa Mwananchi Communications Limited (MCL), Shaban Ndyamukama umesafirishwa kutoka Mwanza kwenda Muleba mkoani Kagera kwa ajili ya mazishi.

Shaban aliyekuwa mwandishi wa MCL wilayani Ngara mkoa wa Kagera alifariki jana Ijumaa Aprili 5, 2019 wakati akipelekwa Hospitali ya Jeshi, Uwanja wa Ndege jijini Mwanza baada ya kuugua ghafla.

Safari ya kwenda Muleba imeanza leo Jumamosi mchana Aprili 6, 2019 katika Hospitali ya mkoa, Sekou Toure jijini Mwanza ambako baada ya kufikwa na mauti, mwili wake ulihifadhiwa.

Ndugu wa marehemu, Faraji Bayasabe amesema iwapo wakifika mapema wataweza kuzika.

"Tunaondoka kuelekea nyumbani kijiji cha Nshisha wilayani Muleba mkoani Kagera na tunatarajia kwamba tukifika mapema kabla ya saa moja, tutazika," amesema.

Amesema marehemu amefariki wakati mtoto wake wa kiume akiwa anaumwa mkoani Pwani.

Familia ya marehemu Ndyamukama, imeshukuru ushirikiano ulioonyeshwa na Kampuni MCL inayochapisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na MwanaSpoti kuanzia utaratibu wa hospitali hadi kusafirisha.

"Kwa kweli Mwananchi tunawashukuru sana kwa mchango wenu, mmekuwa karibu sana nasi na kiukweli tumefarijika sana," amesema Bayasabe.

 



Columnist: mwananchi.co.tz