Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Mwanaume huyu hanionei wivu, hivi ni kweli ananipenda?

Mon, 25 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Nimeolewa na nina watoto watano na mume wangu. Ninafanya kazi , tatizo la mume wangu hata nirudi saa nane na usiku haniulizi.

Siamini kama ananipenda.

Nifanyeje ili nijue kama ananipenda kweli?

Hongera kwa kupendwa na kuonewa huruma, mumeo anakuonea huruma ndiyo maana hataki kukutia presha.

Usichokonoe mambo yaliyolala, inawezekana anaumia roho kama binadamu kutokana na majukumu yako kukufanya muda mwingi uwe nje ya nyumbani, anashindwa la kufanya kwa kujua unatafuta maisha.

Hakuna kitu kibaya kama kumfikiria mwenza wako mambo mabaya, elewa tu anakupenda na amekupa uhuru wa kufanya ukifanyacho.

Anadai hawa siyo watoto wake

Nimeolewa na nina watoto watatu, kitu kinachonikwaza ni mume wangu kila kukicha analalama hawa watoto siyo wake.

Nifanyeje Anti?

Jambo ulilokosea ni kukubali kuwapo kwa hali ya kulalamikiwa na mumeo kuhusu watoto wenu bila kuchukua hatua ya kulikomesha kama siyo kulimaliza jambo hilo ikiwezekana kwa kuwashirikisha baadhi ya wanafamilia.

Ikishindikana kabisa mwambie mumeo akawapime vinasaba (DNA) kujiridhisha kama siyo watoto wake au ni wake.

Ila mjitahidi kujiridhisha mnapotaka kuwapima watoto wasijue kwa sababu inaweza kuleta picha tofauti.

Katika kesi kama hiyo wanaoathirika zaidi ni watoto iwapo itabainika siyo wa kwake watamchukia mama yao maisha yao yote na hawatamuamini tena, na ikibainika ni wake watamchukia baba yao.

Mama na mke wangu wanagombea nini?

Anti sijui nianzie wapi jinsi ninavyopata wakati mgumu wa kuamua kesi kila kukicha kati ya mama yangu na mke wangu.

Sijui mwenye tatizo ni mama yangu au mke wangu, kwa sababu kabla hatujaamua kuishi na mama hapo nyumbani, walikuwa wanapendana na kuelewana.

Pole sana, sidhani kama ulitumia busara kuwaweka pamoja mama na mkeo, kwa sababu mama wakwe na wanawake walioolewa miaka na miaka wamekuwa na uhasama usiokuwa na sababu.

Ukikuta wanaelewana ujue wanaishi mbalimbali, wanaoishi pamoja wengi hawaelewani.

Hilo moja, pili kosa kubwa analo mkeo kwa sababu hata iweje huyo ni mama yake na anapaswa kumuheshimu, na kuvumilia mapungufu yake. Itisha kikao cha familia kama una ndugu, kinachohusisha na ndugu wa mkeo halafu uwasikilize kwa pamoja na uwapatanishe kwa viapo .



Columnist: mwananchi.co.tz