Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Music Facts: Mambo 7 ya kusimulia rafiki zako kuhusu Iyena ya Diamond na vionjo vya Zari (+Audio)

Video Archive
Mon, 4 Jun 2018 Chanzo: bongo5.com

Diamond Platnumz kutokea WCB kwa sasa anachukua headlines zake za kutosha mara baada ya kuachia ngoma yake mpya ‘Iyena’. Uzitoka wa ngoma hii umekuja baada ya kuonekana kwa aliyekuwa baby mama wake, Zari The Boss Lady.



Leo June 03, 2018 kupitia Music Facts ya Bongo5 nakudondoshea mambo saba ya kawaida kabisa kuhusiana na wimbo huo ‘Iyena’ kisha kawasimulie rafiki zako.

1. Wimbo ‘Iyena’ ni wa pili kwa Diamond kumshirikisha Rayvanny baada ya Salome. Wimbo huu Queen Video ni Zari The Boss Lady ambaye amezaa watoto wawili na Diamond, pia katika ya video ya Salome, Queen Video ni Hamisa Mobetto ambaye pia amezaa na Diamond mtoto mmoja.

2. Video ya wimbo Iyena ni ya pili kutoka official katika albamu ya A Boy From Tandale. Video ya kwanza kutoka ilikuwa ni ya wimbo African Beuaty ambayo Diamond amemshirikisha Omario kutoka nchini Marekani.

3. Kwa taarifa yako video ya wimbo ‘Iyena’ ni ya pili kwa Zari akitokea kama Queen Video. Video ya kwanza ni Utanipenda ambayo ilitoka December 11, 2015 na Diamond alieleza kuwa alimlipa Zari kwa ajili ya kazi hiyo ila bado haijajulikana kama amefanya hivyo tena.

Kingine ni mama mzazi wa Diamond naye pia ametokea katika video zote mbili, huku kwa namna moja au nyingine akicheza kama mama mkwe kwa upande wa Zari.

4. Kama nilivyotangulia kueleza kuwa wimbo ‘Iyena’ ni wa pili kwa Diamond kumshirikisha Rayvanny baada ya Salome. Stori hapa ni kwamba video ya Iyena imefikisha views milioni 1 ndani ya saa 19 katika mtandao wa YouTube, wakati Salome ilifanya hivyo ndani ya saa 48 (siku mbili).

5. Bado tupo na namba nne; katika video hizo mbili (Iyena na Salome) kuna couple mbali zilizojitokeza. Ishu ni kwamba katika ya Salome, Harmonzie na Wolper walitokea kama couple ila sasa wameachana, pia katika video ya ‘Iyena’ Diamond na Zari wametokea kama couple na kwa sasa wameachana pia.

Come on point; Mose Iyobo na Aunt Ezekiel ndio couple pekee iliyotokea katika video zote mbili na hadi sasa inaendelea kupeta.

6. Kama utani vile ila ndivyo ilivyo; katika video ya Iyena Zari ametokea na nguo tano tofauti, wakati Diamond ametokea nne tofauti.

7. Wimbo wa Iyena unatoka zikiwa ni siku 106 zimepita tangu Zari The Boss Lady atangaze kuachana na Diamond. February 14, 2018 siku ya wapendanao (Valentine Day) ndipo Zari alitangaza kuvunja mahusiano yake na Diamond kwa kile alichodai muimbaji huyo anamvunjia utu wake katika mitandao kwa kuwa na wanawake tofauti tofauti.

Loading...
Columnist: bongo5.com