Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Mtaalamu: Simba hukaa fungate

66631 Pic+simba

Sun, 14 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kila wanyama wana utaratibu wao wa kukutana kwa ajili ya kuanzisha familia, lakini wa simba ulishangaza wengi hasa waliposikia huwa wanakaa fungate.

Hii ilisikika juzi katika mazungumzo baina ya Ally Salum ambaye ni mtaalamu kutoka Maliasili na wananchi waliotembelea banda la simba lililopo katika Viwanja vya Sabasaba Dar es Salaam.

Mtaalamu huyo alisimulia namna wanyama hao wanavyoishi, wanavyowinda na hata wanavyokutana pindi simba jike anapokuwa katika joto.

Akizungumza katika maonyesho ya 43 ya biashara kimataifa, Salum alisema simba dume mmoja humiliki majike kati ya manane hadi tisa na hakuna dume mwingine atakayeingia kwenye himaya yake kwani zaidi ya hapo ni vita isiyozuilika.

Alisema wanapotaka kukutana wanakuwa na siku zao maalumu za fungate ambazo hakuna kuwinda, kula wala kunywa. “Kabla ya kuingia kwenye fungate hiyo, simba jike hutafuta chakula cha kutosha kwa ajili ya simba dume ili ale ashibe kwa ajili ya kuingia mafichoni.

“Wana kawaida kwamba jike anapokuwa katika joto ndiye anayemfuata mwanaume kwa ishara mbalimbali kama kumpiga ama kumtikisia mkia,” alisema Salumu.

Pia Soma

Pia, alisema simba jike anapowinda kwa ajli ya dume siyo kwamba dume hawezi bali mara nyingi majike wanaonyesha mapenzi kwa madume hayo.

“Simba jike wana mahaba sana kwa madume, hawapendi wateseke, hivyo siyo kama hawajui kuwinda ila ndiyo utaratibu wao kwamba wao waletewe na majike; hiyo ni moja ya mapenzi tu lakini akizeeka sana anaanza kuwinda mwenyewe,” alisema.

Mtaalamu huyo anayetunza simba hao alisema simba baada ya kupata mimba huibeba ndani ya siku 110 na huzaa watoto wa tatu hadi wanne.

Columnist: mwananchi.co.tz