Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Moto aliouwasha JPM ukazimikie Cameroon 2019

23487 Ibra+Bakari TanzaniaWeb

Mon, 22 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ilishuka dimbani Jumanne iliyopita kucheza na Cape Verde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ikiwa ni mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Afrika 2019 zitakazofanyika Cameroon. Timu hizo zilirudiana baada mchezo wa kwanza Cape Verde kushinda mabao 3-0.

Stars iko Kundi L pamoja na Uganda na Lesotho.

Tanzania inawania kucheza Fainali za Afrika mwakani na mara zote imekuwa inaishia hatua za awali, lakini kama mikakati ikiandaliwa kikamilifu, nafasi hiyo ipo na inaweza kufika mbali.

Siku mbili baada ya mchezo, baadhi ya wachezaji wa Taifa Stars, walikutana na Rais John Magufuli Ikulu kwa ajili ya kuzungumza nao.

Pamoja na kuilaza Cape Verde mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Rais alisema hakufurahishwa na wala hakushangilia uishindi ule.

Alisema bado hawakushinda kwa kuwa walipigwa 3-0, walikuwa na deni la bao moja.

Inawezekana kuwa iko hivyo, ni kweli na hali kama hiyo inakuwa mbaya kwa mechi za mtoano. Kama ingekuwa mtoano, Cape Verde anasonga sisi tuangaliana kwa jumla ya mabao 3-2.

Klabu za Ulaya zinaweza mapinduzi hayo, zinapigwa tatu na nyumbani mabao yanarudi kama masihara.

Hoja yangu si hapo sana. Ninataka kuangalia ilipoanza kutolewa Sh50milioni kwa ajili ya safari ya Lesotho.

Rais amemwaga mkwanja wa maana akisisitiza uwe kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya Lesotho na zaidi akataka ushindi vinginevyo watazitapika.

Mimi nasema, huo ni kama moto ameuwasha kwa wachezaji, mabenchi ya ufundi, viongozi wa TFF, BMT na wadau kuhakikisha Taifa Stars inakwenda Cameroon mwakani.

Kinachotakiwa ni hima kwa kila hali lazima Lesotho akae ambako ndiko tutapata mwelekeo mzuri.

Inashindikana vipi kama ukipigwa mpira mwingi kama ulivyokuwa kwa Lesotho? Maandalizi yafanyike na ihakikishwe soka linapigwa kwa hali yoyote hadi Lesotho wakae tena kwenye arsdhi yao.

Watakuja Uganda, pia wanafungika. Kama tulifungwa na Cape Verde 3-0 tukatumia uwanja wa nyumbani kumtandika mabao 2-0 inawezekana kwa Uganda mambo yakawa mtereko.

Tunasema mteremko tukiombea washinde mechi yao na Cape Verde ili kukata tiketi ili kuwapunguzia presha mechi yetu kwani watakuwa hawana cha kupoteza.

Uganda tumetoka nao suluhu tena kwao kwenye Uwanja wa Namboole tutashindwaje kuwapiga hapa Taifa?

Inawezekana na ndivyo ilivyo soka iko katika hali tatu lakini Rais hataki kusikia kufungwa hataki kusikia sare, yeye anachotaka ni ushindi.

Moto wake sasa tuukoleze na tukauzime Cameroon baada ya fainali katikati ya Julai mwakani kuona tumefikia wapi. Kwa wale wasomaji wangu, wiki iliyopita nilisema huu ni wakati sasa wa benchi la ufundi kuanza kuwasoma Lesotho mwanzo mwisho.

Ukiangalia mchezo wa kwanza wa Cape Verde hatukuwasoma kabisa na ndiyo maana tulipigwa, lakini angalia marudiano, tuliwasoma na tukawadhibiti hata kuwapiga. Njia zote zilizibwa.

Kuanza kuwasoma sasa Lesotho kutasaidia kwa kiasi kikubwa kocha kufahamu taktiki na tekniki zao, mfumo, aina ya wachezaji, nguvu yao iko wapi na mwisho wa siku wanaingia pale Maseru bila hofu kwa kuwa wameshawasoma, vinginevyo 50m mtazitapika kwa njia yoyote. Watanzania wana kiu ya ushindi na mafanikio zaidi.

Columnist: mwananchi.co.tz