Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Mkulima: Vijana geukieni kilimo hiki msisubiri kuajiriwa

59346 Nmbpic

Fri, 24 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkulima anayelima kilimo kisichotumia udongo, Mwamy Mlangwa amesema vijana wanayo nafasi kubwa ya kubadilisha maisha yao kama watajikita kwenye kilimo hasa cha biashara.

Mlangwa ameyasema hayo leo Alhamisi Mei 23, 2091 kwenye mjadala unaoendelea usiku huu, wa Jukwaa la Fikra lililoandaliwa na Kampuni ya Mwananchi  (MCL) na kufanyika kwenye ukumbi wa Kisenga jijini Dar es Salaam.

Jukwa hili linafanyika ikiwa ni mara ya nne tangu kuanzishwa kwake,  lilianza na sekta ya Afya, Uchumi, Nishati na mjadala wa leo unahusu sekta ya kilimo na kauli mbiu yake  ni ‘Kilimo, Maisha yetu’.

 

Mwamy amesema kupitia jukwaa hilo, anatarajia vijana watabadili mtazamo wa maisha yao kwa kujiajiri kupitia kilimo.

“Mimi nina miaka mitatu sasa tangu nimeanza kilimo hicho kisichotumia udongo, kimebadilisha maisha yangu kwa asilimia kubwa nilijaribu nikaweza naimani wengine hasa vijana nao wataweza,” amesema.

Pia Soma

Kilimo hicho cha kisasa anasema kinatunza mazingira kwa sababu hakitumii ardhi.

Mkulima mwingine wa mbogamboga, Frank Mbagala amesema tofauti na zamani, hivi sasa kilimo ni biashara na ili ufanikiwe, inahitaji kujiwekea mikakati.

Ili ufanikiwe unatakiwa kupitia hatua kuu tatu ambazo ni uandaaji, uzalishaji, ugavi na mauzo,” amesema Mbaga ambaye pia analima matunda Wilaya ya Kibiti,  Mkoa wa Pwani.

 

Columnist: mwananchi.co.tz