Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Mfahamu zaidi pweza mwenye mioyo mitatu

95146 Pweza+pic Mfahamu zaidi pweza mwenye mioyo mitatu

Mon, 10 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Pweza ni moja ya samaki wanaopatikana baharini lakini pia mwenye uwezo wa kuishi nchi kavu. Samaki huyu amepata umaarufu mitaani kutokana na manufaa yake katika mwili wa binadamu.

Pamoja na faida mbalimbali zinazotajwa zinazotokana na samaki huyo maarufu kwa jina la “paka bahari’’ lakini yapo mambo mengi ambayo hayafahamiki kwa walaji wa kitoweo hicho.

Pamoja na mambo mengine yanayotajwa kuhusiana na pweza lakini moyo wa pweza unaweza ukawa kitu cha ajabu kwa wengi.

Moyo unafanya kazi ya kusukuma damu katika mwili wa kiumbe hai. Moyo unaposimama kiumbe hai anapoteza uhai wake. Binadamu na viumbe wengine wana moyo mmoja katika mwili wake.

Kitu ambacho si cha kawaida na ambacho huenda walaji wa pweza hawakifahamu ni kwamba Pweza ana mioyo mitatu.

Kwa wale wanaoishi ukanda wa Pwani watakuwa wanafahamu umbo la pweza lakini kwa wale wengi wanaoishi maeneo ya bara wanaposikia pweza hujiwa na picha mbalimbali za umbo la kitoweo huyo.

Pia Soma

Advertisement

Kiuhalisia samaki huyu hana umbo la kutamaniwa kuliwa lakini wengi wakimuona pweza hupata kinyaa na kushindwa kumla, baadhi ya watu wa bara wanapotembelea maeneo ya Pwani mfano mikoa ya Tanga, Pwani, Dar es Salaam na visiwa vya Zanzibar wanakuwa na shauku ya kumla pweza kutokana na umaarufu wake.

Kutokana mwonekano wa umbo lake wa kuwa na kiwiliwili kidogo na mikia mingi kama kichane cha ndizi wengi wanamnasibisha na masuala ya kishirikina.

Yapo manufaa mbalimbali ambayo yanatokana na samaki huyo ambayo yamethibitishwa na tafiti za kitabibu na lishe lakini pia zipo faida ambazo zinatokana na Imani.

Samaki huyu amejipatia umaarufu mkubwa kutokana na wengi kuamini anaongeza nguvu za kiume.

Wataalamu wa afya na lishe wanabainisha pweza ana zaidi ya virutubisho 12 vinavyopatikana kwenye supu au minofu ya samaki huyo ikiwamo protini, mafuta vitamini, selenium, madini chuma na shaba.

Virutubisho hivyo vinavyotokana na minofu na supu ya pweza vinaaminika vinavyosaidia kwa kiasi kikubwa kuwapa nguvu ya tendo la ndoa wanaume na wanawake, kuongeza maziwa kwa wanawake na kuongeza madini joto mwilini.

 

 

Columnist: mwananchi.co.tz