Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Mdau: Rayvanny baada ya kuondoka WCB, afanye hivi ili asipotee

Harmonize And Rayvanny Rayvanny na Harmonize

Fri, 15 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sometimes Lebo huwa zina hasara zake maana mara nyingi unakuta watu wanashabikia lebo wala sio wasanii wa lebo hiyo.

Kiufupi ni kwamba Zuchu hana mashabiki, LavaLava hana mashabiki, Mbosso hana mashabiki, Queen Darlin hana mashabiki na huyu Rayvanny hana mashabiki bali hawa wote wapo chini ya muamvuli wa mashabiki wa WCB/ DIAMOND PLATNUMZ.

Hivyo ili utoke WCB na ufanye vizuri zaidi ni lazima utofautiane kwanza na WCB ili Watu ambao sio Mashabiki wa WCB wakuunge wewe mkono wakijua kwamba ipo siku utawashinda maadui zao.

Hii njia ndio ilimuokoa Harmonize, jamaa alilialia sana baada ya kutoka WCB hivyo akadaka mashabiki wote wa Alikiba kisha akadata Wapinzani wote wa WCB, wakawa mashabiki zake.

Kama huamini hili fatilia mashabiki wa Harmonize huwa hawataki kabisa kusikia kuhusu WCB, HIKI KITU NDIO KINA MBEBA SANA HARMONIZE NA HARMONIZE ANALIJUA HILO NDIO MAANA HATOKUJA KUKAA MEZA MOJA AKAELEWANA NA WCB.

HATA ALIKIBA ANAJUA HILI SIKU AKIELEWANA NA DIAMOND MUZIKI WAKE NDIO UTAKUWA BASI TENA.

Cha kumshauri Rayvanny ni kwamba achague ngome moja ya kushindana nayo, aidha WCB au KONDE GANG. Ila akikaa kizembe kama Mavoko tutamsahau muda si mrefu.

Columnist: www.tanzaniaweb.live