Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Mazoezi 4 muhimu ya misuli ya tumbo soma hapa

11778 Mazoez+pic TanzaniaWeb

Thu, 19 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

KAMA ipo sehemu moja ya mwili ambayo ni sumbufu sana kuonyesha matokeo baada ya mazoezi ya muda wa kama wiki kadhaa au miezi  ni eneo la tumbo hadi kiunoni.

Mhusika anaweza akashiriki mazoezi makali kwa wiki kadhaa au hata miezi na sehemu zingine za mwili zikawahi kuonyesha matokeo kwa kipindi kifupi ila sio tumbo au eneo la kiunoni.

 

KWA NINI IWE HIVYO?

Hii ni kwa sababu misuli ya eneo la tumbo hadi kiunoni huhitaji mazoezi maalumu. Huwa na mazoezi magumu zaidi yakilinganishwa na yale ya viungo vingine vya mwili.

Ili misuli ya tumbo na kiunoni kuungika na kuwa dhabiti, utahitaji subira ukitakiwa kutokataa tamaa na kuendelea na ratiba ya mazoezi.

Hii ndio sababu mtu anapofanikiwa kuzipata 6 pack, zipo dondoo za mazoezi anazoshauriwa kuzingatia kufanya kila siku kwa dakika tano baada ya mazoezi ya siku ili kuhakikisha unakuwa imara.

Haya ni mazoezi yanayopaswa kufanywa kila siku kwa dakika tano baada ya mazoezi kwenye ratiba ya siku. Mazoezi haya hayahitaji mashine hivyo yanaweza kufanyiwa kokote. Husaidia sana kudumisha udhabiti wa misuli ya tumbo.

 

1. Crunch: Tandaza mkeka kisha ulalie ukitizama juu. Pumua hewa ndani kisha jinyanyue kutoka sakafuni ukitumia mgongo wako huku sehemu yako ya chini kuwanza makalioni ikisalia sakafuni. Toa hewa nje kisha rudi kwenye pozi ya kwanza na urudie. Endelea kwa dakika 1.

 

2. Crunch with Knee Up: Zoezi hili ni kama tu la kwanza ila tofauti ni kwamba hapa utatakiwa kunyanyua miguu yako kwa angle ya 45 digrii muda wote na unapokuwa ukinyanyua mabega yako. Endelea kwa dakika 1.

 

3. Oblique V-up: ukiwa umelala chini nyanyua mguu wa kushoto na uweke juu ya wa kulia ukiwa umekunja goti la mguu huo. Mkono wa  kushoto uweke nyuma ya kichwa. Ukiwa kwenye pozi hiyo jinyanyue huku ukijisapoti na kalio la kulia na kubana tumbo huku ukileta mguu wako wa kulia uliobeba wa kushoto karibu na kifua. Kisha jikunjue na kurudi kwenye pozi laa kwanza.

Rudia kwa dakika 1, kisha badilishia ule mguu mwingine na upige tizi hiyo tena kwa dakika 1 vilevile.

 

4. Plank Hip Dip: Ukiwa kwenye pozi la push up vile huku ukiwa umekunja mikono yako, hakikisha miguu yako nayo ipo pamoja. Taratibu pindisha kiuno chako kwenda kushoto na kisha rudi hadi katikati na tena uupindishe kwenda kulia wakati wote miguu yako ikiwa imebanana pamoja. Piga tizi hiyo kwa dakika 1.

 

KUMBUKA

1. Hupaswi kupumzika wakati wa mazoezi haya. Unapaswa kufululiza. Kwa matokeo bora zaidi unaweza ukafanya mara mbili (itakayokuwa dakika 10 kwa jumla).

 

2. Zingatia suala la lishe bora. Hii ina maana kuwa utahitajika kuwa mbali na vyakula vyenye kabohydreti nyingi na sukari. Zingatia zaidi vyakula vya proteni.

Columnist: mwananchi.co.tz