Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Maradhi ya Figo na faida za kufunga kula - 3

44649 Fredy Macha Maradhi ya Figo na faida za kufunga kula - 3

Tue, 5 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Suala la kufunga limeanza kuenea sana huku Uzunguni.

Wengi Tanzania ( na hata Ughaibuni) tunavyosikia nahau “kufunga kula” huihusisha na Uislamu au mwezi mukufu wa Ramadhani tu. Basi. Hatuelewi kuwa dini ZOTE duniani zina kipengele cha kufunga kula. Wanaofuata kanuni hizi kwa dhati huwa zaidi Waislamu na Wayahudi. Wengine tumesahau au tunakiuka masharti.

Pili, kupo kufunga kwa mitindo kadhaa.

Mara kwa mara mfungo wa kidini ni wa saa 24 tu. Ufungaji wa aina ya pili ni ule unaopumzisha viungo vya ndani na kuusafisha mwili, kwa siku chache huku mtu unakunywa maji au huli chochote. Tafiti mbalimbali za kisayansi zimeshaweka wazi faida za kufunga kula .

Imegundulika mazoea ya kutokula kati ya saa 36-72 ( yaani siku moja hadi tatu), kila mwezi au miezi miwili, huwa na faida tano kuu : kuongeza urefu wa maisha yako, kupunguza madhara ya vyakula vibovu tunavyokula –kama sukari, pombe, sigara, kahawa na sumu nyingine zilizoko katika milo.

Nyama , mathalan, ina protini na madini lakini pia ina sumu ikiliwa kila siku (mafuta yake na ngozi ni mbaya, kwa mfano).

Vyakula vyenye vikolezo vikali (“spices”) huchosha figo: pilipili, binzari, chumvi, nk. Vikolezo au viungo hivi ni muhimu mwilini. Binzari huchangia kupambana na maradhi (“anti oxidants”), na uchafu wa mazingira (“free radicals”). Ila si vizuri kula vikolezo vya aina moja kila mlo au kila siku. Unapokula kitu kilekile kila siku (kama tulivyoona makala mbili zilizopita) unatesa au kuhizisha figo na ini lako.

Tatu, kufunga husafisha mwili na kiwili wili kizima, kupitia mifupa, viungo, ngozi, harufu ya tumbo (na mdomo), kucha na nywele. Ndiyo maana ukifunga ngozi husafishika na kunawiri.

Kwa vipi?

Unapofunga mara ya kwanza, (kama hukuzoea) utajisikia vibaya sana (hii ni kutokana na virusi rafiki mwilini kupambana na virusi vibaya). Kufunga husababisha virusi vibaya kukosa chakula na kushambuliwa na virusi rafiki mwilini.

Nne, kufunga huweka uwiano wa sukari katika damu. Imedhihirika ukifunga unapunguza uwezekano wa kupatwa maradhi ya kisukari, kiharusi (presha ya moyo) na maradhi mengine yanayohusiana na damu. Pia unapunguza unene.

Mwisho, ukifunga unapumzisha ubongo, hivyo fikra zako zinakuwa pevu. Ni kitendo kizuri sana kujenga siha ya ubongo kwa kusaidia kufikiri na kuongoza mwenendo mzima wa mwili. Ubongo huwa kazini kila saa hata tunapolala.

Unapokula kazi kuu ya ubongo ni kuhakikisha chakula kinasukumwa kila inapotakiwa : hadi kutolewa nje (kinyesi). Kula ni kazi kubwa inayochukua nafasi au muda mwingi sana. Unapofunga ubongo hupata ahueni.

Mapumziko ya ubongo hukujenga kiroho na kiibada na ndivyo waumini wa dini wanavyofaidika. Hukupa nafasi ya kuwasiliana vizuri na Mola wako.

Na ndiyo maana mitume wakubwa wa zamani (na hata viongozi au watunzi mahiri wa kisayansi na kisanaa leo ) hufunga mara kwa mara. Kufunga ni kutuliza roho na mwili.

Kabla ya kufunga hakikisha umepimwa na mganga. Kwamba huna matatizo makubwa kama kifafa, maradhi ya figo, ini, moyo au ubongo.

Tumalizie mada wiki ijayo.



Columnist: mwananchi.co.tz