Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Mambo ya kuzingatia Tazara flyover

18380 Tazara+pic TanzaniaWeb

Fri, 21 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Watumiaji wa vyombo vya moto wametakiwa kuzingatia mambo manne katika barabara ya juu ‘flyover’ iliyopo makutano ya Barabara za Nyerere na Mandela (Tazara).

Barabara hiyo ilianza kutumika siku tano zilizopita kwa madereva wa daladala, magari binafsi na usafiri wa bodaboda huku wachuuzi wa biashara ndogo wakilalama kukosa wateja waliotokana na foleni. 

Miongoni mwa mambo yaliyozuiliwa na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) ni pamoja na dereva wa gari kutumia mwendokasi unaozidi kilomita 40 kwa saa anapopanda flyover hiyo.

Pia, watumiaji hao wametakiwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za usalama barabarani, zilizopo kwa wakati wote ikiwamo dereva wa gari kutosimama katikati ya barabara hiyo ya juu.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tanroads, Mhandisi Patrick Mfugale ameliambia gazeti hili leo Septemba 20, 2018 kwamba, barabara hiyo iliyogharimu Sh100 bilioni, itakuwa na uwezo wa kubeba tani 180 tu kwa wakati mmoja. 

“Haitakiwi kuzidi zaidi ya tani hizo kwa wakati mmoja na uhai wake ni miaka 100, ndiyo ijengwe upya,” amesema Mhandisi Mfugale. 

 

 

Columnist: mwananchi.co.tz