Inaendelea kutokea wiki jana
7. Usimlaumu, usimlalamikie wala kumkejeli mumeo anaporudi nyumbani mikono mitupu au anaposhindwa kuhudumia kama alivyotarajiwa tofauti na tabia yake ya kawaida, badala yake mtie moyo ya kwamba unaelewa hali halisi na siku moja hali itakuwa sawa tu. Yamkini mtu mmoja pekee wa kumpa maneno hayo kwenye ulimwengu wake ni wewe tu, usimkatishe tamaa bali uinue moyo wake uliovunjika. Neno lako moja la faraja lina nguvu kuliko maneno 100 ya mtu mwingine. Hata kama amekuwa ana tabia za kutokubeba majukumu vile unavyopenda wewe, fahamu kwamba kejeli, makelele na lawama za mfululizo hazitokupa matokeo mazuri zaidi ya kuja kukuongezea maumivu tu.
9). Kamwe usijifanyishe kuwa unaumwa au una ugonjwa ili tu kumnyima mume wako tendo la ndoa, msaidie kuitimiza kiu yake kwa kadri anavyotamani kwa sababu tendo hilo ni muhimu zaidi kwa mume wako. Kwa kumnyima au kulitumia tendo hilo kama adhabu haitombadilisha tabia na kumfanya awe mwema utakavyo badala yake itamgeuza kuwa mbaya zaidi na kuna uwezekano mkubwa hiyo ndiyo ikawa tiketi yake ya kwanza ya kutoka nje ya mahusiano yenu, ili kutafuta tendo hilo alilolikosa kwako. Fahamu kwamba ni kitu kigumu sana kwa mwanaume wa kawaida aliyeoa na aliyekamilika kukaa muda mrefu pasipo tendo hilo.
10. Kamwe usimlinganishe au kumfananisha mume wako na yeyote ambaye amewahi kuwa mpenzi wako huko awali. Hata kama nia yako ni nzuri ila tafuta mlingano mwingine ila sio na ex wako. Kosa hilo linaweza kuifanya ndoa yako isipone kirahisi kutoka kwenye hilo jeraha. Kuwa makini sana.
11. Najua tunatofautiana utamaduni na namna tunavyoishi kwenye ndoa zetu ila mara nyingi jaribu kuepuka kumsemea mume wako au kujibu kwa niaba yake pasipo ridhaa yake. Acha achukue jukumu la kusema au kujibu kama yeye ndio amehitajika kufanya hivyo, ingawa mara nyingine yeye akisema kwa niaba yako inaweza isilete shida na bado mambo yakaendelea vizuri tu. Kuna mambo kwenye ndoa ni kama gia za gari, hata kama gia namba moja na mbili na tatu zote ni gia lakini lazima uanze na moja uende mbili halafu tatu, sasa unapo lazimisha kuanzia gia namba nne kwa sababu tu gari ni lako unasababisha tatizo kwenye gari na watu watasema dereva wa hili gari ni kichaa.
Pia Soma
- ANTI BETTIE: Nikifanya mapenzi na mwenza wangu ninaumia, nifanyeje?
- USHAURI WA DAKTARI: Kuwa na nguvu za kiume ni kitu kimoja na uwezo wa kutungisha mimba ni kitu kingine
- Mahakama yatengua uamuzi wa msajili wa vyama dhidi ya DP