Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Mambo matano unayopaswa kuyafahamu leo

9837 Mambo+pic TZWeb

Sun, 24 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Picha za Uwoya zazua gumzo mtandaoni

Picha za ufukweni za mwigizaji Irene Uwoya zimezua gumzo mtandaoni wakioanisha na picha zake alizopiga wiki chache zilizopita wakati wa mwezi wa Ramadhan. Muigizaji Mwijaku ni mmoja kati ya watu waliozungumzia picha hizo wakisema haziendani na maadili hasa kwa mwanamke ambaye ni mke wa mtu. Mwigizaji mwenzake, Shamsa Ford amemtetea akisema Uwoya yupo sahihi kwa kuwa picha hizo alipiga ufukweni.

Vipimo vya samaki kwa rula vyaamsha utani

Baada ya sakata la Maofisa wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuingia katika mgahawa wa Bunge na kukagua samaki kwa madai ya kupewa maagizo na Waziri wa wizara hiyo Luhaga Mpina na Spika wa Bunge Job Ndugai kuwataka Wabunge kumsamehe Waziri huyo wananchi waligeuza tukio hilo kuwa sehemu ya utani katika jamii. Katika mitandao vibonzo vya upimaji samaki kwa rula vilitawala.

Canada wahalalisha bangi

Mapema wiki hii nchini Canada wamepitisha sheria rasmi kwa nchi nzima inayoruhusu matumizi ya bangi kwa raia wa nchi hiyo na hata wageni. Sheria imepitishwa kwa kupata kura za ndiyo 52 zinazoruhusu matumizi ya bangi hadharani, huku kura 29 za maseneta.

Kuanzia Septemba mwaka huu raia wa Canada wataruhusiwa kununua na kutumia bangi kihalali . Matumizi ya bangi kama dawa yaliruhusiwa kisheria tangu mwaka 2001.

Kinana aagwa, Dk Bashiru akaribishwa

Wabunge wa CCM waliandaa hafla ya kumuaga aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho Abdulrahman Kinana na kumkaribisha Katibu Mkuu mpya, Dk Bashiru Ally, jijini Dodoma. Katika hafla hiyo wabunge hao walimpa Kinana zawadi ya gari aina ya VOX.

Wasafi TV yaingia Star Times

Moja ya habari kubwa wiki hii ilikuwa chaneli ya Wasafi TV kuingia katika king’amuzi cha Star Times. Katika hafla ya kuitambulisha chaneli hiyo, mmiliki wa Wasafi TV, Diamond Platnumz alisema lengo ni kumfikia kila Mtanzania kwa kumpelekea chaneli hiyo pendwa sebuleni kwake.

Columnist: mwananchi.co.tz