Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Makala: Ni makosa makubwa kushangaa nyimbo za Alikiba kuchezwa Wasafi TV (+Audio)

Video Archive
Fri, 6 Apr 2018 Chanzo: bongo5.com

Rapper Fid Q aliwahi kutema punchline isemayo; Simba kula mtu ni habari ila mtu kula simba ni habari ya kusisimu, ndicho kinachotokea kwa Diamond Platunmz kwa sasa, kivipi?.



Mapema January mwaka huu Diamond aliweka wazi dhamira yake kuanzisha kituo cha Radio na TV (Wasafi TV & FM).

Baada ya Diamond kuweka wazi hilo shauku ikawa ni kubwa kutaka kushuhudia kitu hicho. Kufunguliwa kwa kituo cha Radio au TV si habari ya kushtua ila Diamond kufanya hivyo ni habari kubwa na yenye mashiko kama alivyoeza Fid Q.

Hatimaye usiku wa kuamkia April Mosi mwaka huu wakati wa ugawaji wa tuzo za filamu za Sinema Zetu International Film Festival Award (SZIFF) , Diamond alimueleza Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kuwa Wasafi TV ingeanza kurusha matangazao yake siku inayofuata.

Sekunde sikasonga ikazaliwa dakika, saa zikaenda na siku zikazaliwa na hatimaye leo tunashuhudia kulichokuwa kizungumziwa. Pongezi kwako Diamond.

Kuhusu Alikiba na Wasafi TV

Katika mitandao watu wamepekea kwa ‘mshangao’ mara baada kuona nyimbo za Alikiba zikichezwa Wasafi TV, kiufupi tunaweza kusema baadhi ya watu walikuwa hawaamini kuwa nyimbo za Alikiba zingepewa nafasi hiyo kutokana na ushindani wa wasanii hao kimuziki.

Hata waandishi wa habari hasa wale wa udaku nao wameona nyimbo za Alikib kuchezwa Wasafi TV ni habari yenye mvuto wa aina yake ndio maana baadhi hawakusita kuripoti hilo.

Uchambuzi mashuhuri wa soka nchini, Edo Kumwembe kwenye moja post zake katika mtandao wa Instagram aligusia kwa utani siku moja wimbo Alikiba kushinda nafasi ya kwanza katika chart za muziki ndani ya Wasafi TV baadhi ya watu waliona ni kama ndoto ya mchana kweupe.

Twende mbele twende nyuma, sasa nyimbo za Alikiba zinachezwa je ni habari ya kushangaza au kusisimua?. Hapana, ni makosa kuwa mtazamo huo. Narudia tena, ni makosa makubwa sana. Sababu ni hizi tatu.

Mosi; Wakati Diamond anatangaza siku ambayo Wasafi TV itaanza kurusha matangazo mbele ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alisema wameanzisha kituo hicho kwa ajili ya kutangaza sanaa ya wasanii wa nyumbani

“Mhe. Rais Mstaafu na viongozi wote sisi vijana tunajitahidi sana kuhakikisha hatuwaangushi, tunapopata nafasi hata kama ndogo tunaitumia vizuri sana, tunaamini channel ya Wasafi TV kama nia tuliyoiweka inamilikiwa na wasanii itahakikisha inatangaza sana hasa,” alisema Diamond.



Unapozungumzia kuitangaza sanaa ya nyumbani ni pamoja na muziki wa Alikiba, hivyo nyimbo za Alikiba kuchezwa Wasafi TV ni kwamba Diamond amesimamia kile aliongea mbele ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete.

Pia Diamond angekuwa mtu wa hovyo kupitiliza iwapo angedanganya mbele ya umati wote ule ambao ulijumuisha viongozi mbali mbali wakubwa.

Pili; Licha ya sababu nyingine za kimaendeleo/kibiashara, Diamond ameanzisha Wasafi TV kwa uchungu mara baada ya kubaniwa na baadhi ya vyombo vya habari ambavyo vilisitisha kucheza nyimbo zake na wasanii wake wa WCB.

Hivyo basi Diamond atakuwa mtu hovyo, naomba kurudia tena; atakuwa mtu wa hovyo endapo na yeye atambania msanii mwingine katika chombo chake cha habari. Hivyo mnaoshangaa mnafanya makosa na ningependa kuwapa pole kwa hilo.

Tatu; watu wanapaswa kuelewa kuwa Wasafi TV bado ni chombo kipya cha habari, kinahitaji kujitangaza zaidi. Kitendo cha kucheza nyimbo za Alikiba ni mbinu za kibiashara zinazolenga kulishika soko mapema.

Tunafahamu nyuma ya Diamond na Alikiba kuna makundi makubwa mawili ya mashabiki ambao wanawafuatilia, Hivyo Diamond kupitia Wasafi TV anajua fika mashabiki wake tayari ni wananunuzi wa bidhaa yake, sasa anataka kundi la pili kuwa wateja wa bidhaa yake pia.

Kwa hiyo asipocheza hizo nyimbo za Alikiba kundi hilo la pili atakuwa amelipoteza kwa upande fulani kitu ambacho si kizuri katika mwanzo wa biashara.

Ni Mafanikio ya Bongo Flava

Diamond kuanzisha kitu cha TV na Radio si mafanikio yake pekee yake na team yake ya WCB, laa! hasha, haya ni mafanikio kwa wasanii wote walioipigania Bongo Flava kwa kipindi kirefu na wanaoendelea kufanya hivyo.

Kwanini ni mafanikio kwa wote?, jibu ni kwamba Diamond amepiga hatua moja mbele ambapo waliishia wengine katika upande huo huo wa media, najua bado hujanielewa.

Miaka kadhaa iliyopita baadhi ya wasanii walikuwa na TV Show zao, waliweza kurekodi vipindi vyao na kuvipeleka katika TV Station na kurushwa moja kwa moja.

Utakumbuka Chidi Benz alikuwa na show yake inayokwenda kwa jina la Chidi Show iliyokuwa ikirushwa EATV, pia Fid Q alikuwa kipindi chake kiitwacho Fid Friday Free Style ambacho pia kilirushwa na kituo hicho.

Nitafanya makosa endapo sitamtaja Kala Pina kupitia kipindi chake cha Harakati kinachoruka Clouds Tv, kipindi hiki ambacho kimelenga kuwasaidia vijana dhidi ya kupambana na dawa za kulevya chimbuko lake ni katika ngoma ‘Hip Hop Bila Madawa’ ya Kikosi cha Mizinga.

Mwisho nikumbushe kuhusu msanii pekee wa kike Bongo kuwahi kuwa na TV Show yake, huyu si mwingine bali ni Lady Jaydee kupitia show yake iliyokwenda kwa jina la Diary ya Lady Jaydee iliyokuwa ikiruka EATV.



Turudi katika mada yetu; Tunaposema Diamond amepiga hatua moja ni kwamba ameitoka Bongo Flava pale ambapo wasanii walikuwa wakimiliki vipindi vyao vya TV na kuanza kumiliki vituo vyao vya TV. Kama alivyoanza msanii mmoja kuwa na TV Show kisha wakafuata na wengine bila shaka hata hili Diamond anapaswa kuigwa pia ila katika maana nzuri ya kujenga.

Ulipo Msisimko wa Wasafi TV

Diamond kuja vyombo vyake vya habari imekuwa ni habari yenye msisimko wa aina yake, si kwake pekee, bali hata kwa wasanii wenzake na hasa kwa mashabiki wake.

Mashabiki wake kuna msisimko wa aina yake ambao wanaupata kwa sasa, kwa hali kibinadamu ni vigumu kuuleza nikaeleweka kwa urahisi ila ngoja nikueeleze.

Kama tunavyofahamu kwa sasa kuna baadhi ya vitu vya Radio na TV vimekuwa havichezi kabisa nyimbo za Diamond na wasanii waliochini ya label yake, yaani WCB kwa muda sasa.

Jambo hili limekuwa likiwaumiza mashabiki wa Diamond sana na hata ukiangalia katika baadhi ya mitandao ya kijamii utaona wanavyokuwa wakivishambulia vyombo hivyo. Kiufupi ni kitu ambacho wamekuwa wakichukizwa nacho na wasingependa kuona kikiendelea. Tuachane na hilo.

Haya ni Maoni ya @navykenzoofficial , One of the Greatest Music Group inayopepea vyema Flag Ya Nyerere Land Kwa Dunia!….Mpaka sasa ndio Group na wasanii pekee wa Kizazi kipya kufanya show Nchini Israel…..Chuma Chao kipi Pendwa zaidi kwako? #SanaaImezaliwaUpya #ChomboKwaHewa #HiiNiYetuSote #TumeWasha Cc @aikanavykenzo @nahreel

A post shared by Wasafi TV (@wasafitv) on



Hivyo basi Diamond kumiliki vyombo vyake vya habari ni jambo ambalo limekuja kwa wakati sahihi, mashabiki wake wanaamini wamepata tulizo la hisia zao baada ya kuumizwa kwa muda ingawa bado kuna vyombo vingi vya habari bado vilikuwa bega kwa bega na Diamond.

Mwisho; Mtu yeyote muungwana hana budi kumpongeza Diamond kwa uthubutu wake hadi kufanikisha jambo hilo. Baadhi ya wasanii wamejitokeza  na kumpongeza na watu wakubwa katika media industry nchini wamefanya hivyo, hawa wote ni waungwana. Asante.
Columnist: bongo5.com